Agnes Gerald ‘Masogange’.
AWALI YA YOTEMwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward.
Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!
IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI
Baada ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana.
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea.

IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA
Baada ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage au majina yanafanana tu.
Kamanda huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’.
APIGIWA SIMU
Ilibidi Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa. Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange yule staa.
Kamanda Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.”

JUMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI
Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja.

Toka lini mwizi akiiba anakubali kwamba ameiba?huyo hana jipya anataka kuwapoteza watu lengo tu
ReplyDeleteAnasema yuko huru then anaenda Mahakamani!!!!
ReplyDeletealitaka mwenyew hyo
ReplyDeleteNi madawa ya kulevya asituzuge ni ishu nyingne, pumbafu zake!
ReplyDeleteAsilete uongo hebu pigatena cm yakeuone itapokelewa namashoga zake.ndio yy aliye kamatwa namadawaa asituzuge taarifa tunazo.
ReplyDeleteHILI NDILOTATIZO KUBWA KWA DADA ZETU TAMAA,SASA KAKAMATWA ANATAPATAPA.NABADO MTAKUJA SIKIA NAMWINGINE TENA!!!
ReplyDeleteANYONGWE TU HANA JIPYA HUYO TUMEWACHOKA NA MAVAZI YAO YA NUSU UCHU MPUMBAVU TU HAWANA JIPYA IWE FUNDISHO
ReplyDeleteHapo kuna kamchezo tunachezewa
ReplyDeleteMASOGANGE KITU GANI HATA DEMU WANGU RACHEL ANAYO HAYO MANYAMA HUYU MNAMPA PROMO TU!!!!!!!!!!1
ReplyDeleteBongo bwana!hata manyama uzembe wanaya-mind na kumfanya mtu staa?
ReplyDeletekwa bongo wakati kesi inaendelea ni rahisi kubadilisha kielelezo na kikipimwa na mkemia mkuu utaskia aah! kumbe ni glucose!!! lakini kwa mzee madiba a spade will always be called a spade,masogange huo ni mtihani usiosomeka.
ReplyDeletedruglords inapotokea drugcarrier amekamatwa ni nadra sana kujitokeza kwa nia ya kumsaidia. kwa wenzetu kesi itachukua muda mfupi na kielelezo hakitabadilika kuwa unga wa ngano, so, masogange has a huge mountain to climb, ajipange. ni mimi mzee wa missed call wa tudarco.
ReplyDelete