Sakata la kodi ya umiliki wa kadi za simu (simcard tax) sasa limekuwa personal kati ya waheshimiwa.
Mbunge wa Ubungo, Mh. John Mnyika ametoa kauli ndefu kuhusu sakata hilo,
na kutoa namba za simu za mikononi za baadhi ya waheshimiwa, akiwemo
Mh. January Makamba, hadharani ili wananchi wanaotaka kutoa dukuduku
lao, wawasiliane nao. Inaonekana makubwa yamemkuta mh. Makamba kufuatia
tendo hilo. Angalia alichopost Mh. January Makamba katika mitandao ya
Twitter na Facebook hapa chini kuona yaliyomsibu baada ya wananchi
walionuna kuhusu simcard tax kupata namba yake ya simu:
Facebook:
kauli hiyo ya mh. Mnyika hii hapa chini:
Kufuatia kauli za
Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu;
nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba
zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni
kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa
chafu.
Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana
tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba “Mnyika
anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea
namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao
huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:
Nieleze
kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo
itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha
walau kidogo kwa maendeleo.
Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio
kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na
kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya
siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee
inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Ambacho
sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema
uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu
suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza
kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha
jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii.
Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya
fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga
ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.
Aidha,
sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa
mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya
kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote
zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta
ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub
sector) nyeti ya mafuta.
Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye
mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo
hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya
Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya
kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na
ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya
Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge
walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio
kuipitisha?
Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo
tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita
kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi
nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba
anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima
litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri
akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha
kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati
maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa
kodi hiyo katika mkutano ujao?
Wakati Naibu Waziri akisema hayo,
Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa
kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la
Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania
kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila
laini ya simu za kiganjani.
Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali
inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi
kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644.
Aidha,
ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa
kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake
aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa
majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la
marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.
Nasisiza
kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni
za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi
hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala
ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine
mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha
mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa
Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.
Majina ya
wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika
mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika
Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni
nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na
kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge
hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.
Uongozi
bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji
endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
Ngoja niandike kwa kiswahili fasaha ili mtanzania wa kawaida anielewe ukisikia kufilisika kwa fikra kwa waongozaji nchi na upumbavu wa akili wa washauli wa serikali na kutokuwa na uzalendo wa kiloho na kutowafikilia wananch wa chini ndio kutapelekea kuliangamiza taifa maskini kuwa fukala hii codi ina maana gani ndio taifa la kwanza kusikia upumbavu usiokuwa na fikra kwa wananch waishio chin ya dollah moja au mbili atapa fursa sawa amkeni nyie walala vitini kwenye vikao vya bunge
ReplyDeleteKwa Kweli serikali yetu haitufai tena tabaka la chini ndilo linalonyonywa kila kukicha tumeona wawekezaji wangapi wanasamehewa kodi kipuuzi ila Mtanzania mwenye maisha duni ndio afidie kodi zinazopotea! Mtanzania aishie chini ya dola moja anakutana tena na kodi ktk mawasiliano kiasi cha sh 1000 Watanzania wamechoka Hakuna Maisha bora ila Imekuwa bora Maisha, Mgimwa na Makamba angalieni haya Maswala watanzania waliwaamini wakawapatia kura mkaingia vitengoni muwasaidie!
ReplyDeleteHii Nchi bure kabisa viongozi wanawaza juu ya matumbo yao Bure kabisa dalili za Mvua ni Mawingu CCM kwisha habari Jimalizeni Completely.
ReplyDelete