Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Transparency International,
Kenya imeshika nafasi ya nne kwa ufisadi ikiwa ni miongoni mwa nchi 107
ambako utafiti huo ulifanywa.
Ripoti hiyo ilibaini kwamba Wakenya saba kati ya
10 waliohojiwa walisema wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze
kupata huduma moja hadi nane kati ya zilizochunguzwa.
Kulingana na utafiti huo, maofisa wa polisi ndio
waliopatikana kuwa mafisadi zaidi nchini wakifuatiwa na wabunge, vyama
vya kisiasa, mahakama na wafanyakazi wa Serikali.
Wakenya wengi walisema vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini hazina ufisadi mwingi.
Nchi fisadi zaidi duniani ni Sierra Leone ambako
asilimia 84 ya watu waliohojiwa walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra
Leone inafuatwa na Liberia (asilimia 75) na Yemen (asilimia 74).
Nchi ambazo zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni
Finland, Japan, Australia, Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay,
Norway, New Zealand, Korea Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95
kati ya 100 waliohojiwa walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao.
Katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi
fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda (asilimia 61) na Tanzania (asilimia
56). Kulingana na utafiti huo ambao watu 114,000 walihojiwa, Rwanda
ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.
Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo walikubali mwamba wametoa hongo.
Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi barani Afrika. Baadhi ya nchi
fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji, Libya na Cameroon (zote
zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia 44).
Hizi data za Tz si za kweli hapa yatakiwa kuwa kwenye 70+%
ReplyDelete