MAAJABU:MWANASHERIA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU

Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . 
Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .

Indidis anasema kuwa ushahidi uko kwenye kitabu kitakatifu Cha Biblia ambayo kila mmoja anafahamu kuwa haisemi uongo . Kwa kuwa wafalme na watawala waliohusika na kitendo hicho hawako hai serikali ambazo mipaka yake ndio ile ile ya iliyokuwa falme ya Roma iliyokuwa madarakani kipindi hicho zitawajibika kwa niaba .
Dola Indidis anasema kuwa vitendo alivyofanyiwa Yesu ni vitendo vya kinyama na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nay eye kama mwanadamu anahisi kuwa ni jukumu lake kulinda na kutetea heshima ya Yesu Kristo.

Hata hivyo msemaji wa mahakama ya Dunia ambaye hakutajwa utambulisho wake amesema kuwa hakuna kipengele cha kisheria ambacho kinaweza kuruhusu kusikilizwa kwa kesi hiyo kwani ICJ (International Court Of Justice) husikiliza kesi zinazohusu nchi dhidi ya nchi nyingine hivyo kesi hiyo haiwezi hata kufikiriwa . Indidis kwa upande wake bado ana imani kuwa ana kesi ya kuhoji na anaamini kuwa atashinda kesi hiyo.


Source: MillardAyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad