OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na mapaparazi wa Global
Publishers inazidi kufichua ‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana
na machangu ambao wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio
cha kutafuta fedha za kununulia futari.
‘Askari’ wa OFM, wiki iliyopita alifanya uchunguzi katika viunga
mbalimbali maarufu kwa biashara hiyo na kukuta machangudoa wakifanya
biashara yao kama inavyokuwa katika miezi ya kawaida.
Maeneo ambayo
yalionekana kushamiri zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya
Mwananyamala Hospitali, American Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja
vya Leaders Club, Taasisi ya Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya
Agha-Khan, New Maisha Club (Masaki) na Coco Beach.
Idadi kubwa ya wadada hao walipohojiwa na paparazi wetu, walisema
wanaendelea na biashara hiyo kwa kuwa ndiyo waliyoizoea kutafutia kipato
na wakiiacha, watakufa kwa njaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu
wa Ramadhan.
Ili kujiridhisha kwa data, paparazi wetu alijifanya
mteja na kukutana na machangu wa Makaburi ya Kinondoni ambao walidai
wanapenda waitwe ‘scraper’ au vyuma chakavu pasipo kufafanua zaidi,
bahati mbaya wakashtukia mchezo:
Changudoa: “We kaka mbona
unatuzingua? We ulivyokuja si ulijifanya mteja, kumbe paparazi, sisi
hatuwezi kuacha kujiuza kwa kuwa ndiyo kazi tuliyoizoea, sasa tukikaa
nyumbani tutapata wapi futari?” alihoji mmoja wa machangudoa.
Paparazi: “Hivi ni kweli nyie mnafunga?”
Changudoa: “Wewe tumia ubongo na maswali yako yanayotia njaa, hata kama
sisi tunafunga au hatufungi tuna watu wanaotutegemea majumbani kwetu
kuwatafutia futari, sasa tusipohangaika itakuwaje?”
Baadhi ya
waumini wa dini ya Kiislamu waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walionesha
kukerwa na tabia hiyo na kulaani vibaya kwani mwezi huu ni maalum kwa
ajili ya kumrudia mwenyezi Mungu na kuacha dhambi.
Source:Global Publisher
MACHANGU" TUNAENDELEA KUJIUZA MWEZI MTUKUFU ILI TUPATE HELA YA FUTARI"
3
July 16, 2013
Tags
Tuepushe na maibilisi watu hawa
ReplyDeleteInallilah waina ilaih rajiuun. Madada zetu wamepotea na watajibu nini kwa mola wao. Dunia tunapita. Moto na pepo vinatungojea
ReplyDeletesiyo kinadada tu kwani hao wateja wao ni kina nani?
ReplyDelete