TUME ya Abbottabad imesema kuwa Osama bin Laden aliishi kama mtu wa
kawaida bila wasiwasi wowote kwa karibu miaka 10 na aliwahi hata
kusimamishwa na polisi katika eneo la Swat huko Pakistan kwa kupeleka
gari kwa kasi mno, lakini hakukamatwa.
Ripoti hiyo iliyofichuliwa na Televisheni ya al Jazeera na kuoneshwa
juzi jioni, inaonesha kinagaubaga maelezo ya kusisimua kuhusu maisha ya
Osama bin Laden, mtu hatari aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na
aliyekuwa akivaa kofia la mchunga ng’ombe katika tambarare za Marekani,
kuepuka kugunduliwa kutoka angani.
Ripoti hiyo ya kurasa 336, iliandikwa na tume ya Abbottabad
inayoongozwa na jaji na iliyoundwa na Serikali ya Pakistan muda mfupi
baada ya vikosi maalumu vya Marekani kumuua bin Laden Mei 2 mwaka 2011.
Misingi ya ripoti hiyo ni mahojiano yaliyofanywa na vyanzo 201, wakiwemo
jamaa wa familia yake na maofisa mbalimbali.
Matokeo ya uchunguzi huo ambayo hayajachapishwa rasmi, yanajumuisha
ushahidi wa uzembe mkubwa katika karibu kila ngazi ya vyombo vya usalama
vya Pakistan.
Ripoti inakosoa vikali namna Marekani ilivyofanya uvamizi katika
makazi ya bin Laden huko Abbottabad, ikisema ilichukua hatua kama
jambazi mhalifu. Inauweka katika kiti moto utawala wa Pakistan kwa
kushindwa kugundua shughuli za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA),
katika ardhi yake, na hautupilii mbali uwezekano wa kuhusika maofisa
walaghai katika idara ya ujasusi ya Pakistan, suala tete kuligusia
katika uchunguzi wa hali ya juu namna hiyo.
Ripoti inatoa maelezo kuhusu usiku wa kifo cha bin Laden na kutoa
taswira ya mtu aliyekuwa akibabakia na kama mwenda wazimu ambaye kila
mara alikuwa mbioni kukwepa kutiwa mbaroni.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Bin Laden aliwasili nchini Pakistan msimu
wa machipuko mnamo mwaka 2002, na wakati mmoja aliishi Haripur kwa miaka
miwili kabla kuhamia katika makazi yake ya mjini Abbottabad na familia
yake kubwa mnamo Agosti 2005.
Ripoti inasema maeneo yote alikoishi hayajulikani kikamilifu, lakini
miongoni mwao ni FATA yani Waziristan kusini na Bajaur, Peshwar, Swat na
Haripur.
Ripoti imegundua bin Laden aliingia Pakistan akitoa eneo la Tora Bora
nchini Afghanistan, ambako majeshi ya Marekani yalikuwa yakimsaka mwaka
2002. Familia yake ilihamia Karachi, Pakistan kutoka Kandahar, muda
mfupi baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani dhidi ya
jengo la Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mjini New York, makao
makuu ya wizara ya ulinzi, Pentagon nje ya mji wa Washington, na uwanja
mmoja huko Pennsylvania.
Osama hakupenda mali
Katika ushuhuda wao wake wa bin Laden walisema hakupenda sana mali
zake binafsi na alikuwa na nguo chache sana. Ripoti hiyo imesema kabla
kwenda Abbottabad bin Laden alikuwa na mavazi matatu ya kitamaduni
yajulikanayo kama shalwar kameez aliyoyavaa wakati wa msimu wa kiangazi
na mengine matatu kwa ajili ya msimu wa baridi.
Wakati alipojihisi anaugua, Osama bin Laden alijitibu mwenyewe
kutumia dawa za kienyeji za Kiarabu. Kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi
za Marekani, bin Laden alikuwa akiugua ugonjwa wa Addison, upungufu wa
adrenalini mwilini, na kila mara alipojihisi mvivu angekula tufaha na
chokoleti.
Maofisa wa Serikali na usalama nchini Pakistan hawakuweza kupatikana
ili kutoa kauli kuhusu ripoti hiyo. Baadhi ya maofisa wa Marekani
wameelezea wasiwasi wao wakiyashuku mashirika ya ujasusi ya Pakistan kwa
kumlinda bin Laden, lakini Pakistan imelipuuzilia mbali wazo hilo.
huyu jamaa kama kufa amefariki 2 mwenyewe..ingekuwa ni kweli hawa marekan walimkmata wangemtembeza dunia nzima
ReplyDeleteSiamin kweli kama marekan ilimuua osama kwan hakuna ushahid wowote ulioonekana.hata hivyo vitendo wanavyofanya amerika vya mauji kuanzia sadam,osama na wengine na kufunga watu wengine wasiokua na hatia huko gerza la gwantanamo nchin cuba ni dhambi kubwa na ipo siku watasimama kujibu mbele ya haki
ReplyDeleteinawezekana ni yy walie mkamata,maana asingekaa kimya hivyo,jamaa wako fit sana hawana 7bb zakudanganya.
ReplyDeleteInatakiwa iwepo siku ya Osama Duniani, maana ili tuwe tunakumbuka alikufa lini.
ReplyDeleteHahahahahaaahahahaha!!
Delete