WATUHUMIWA wanne wa ujambazi uliotokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha majeruhi wamekamatwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam Ally Mlege alisema majambazi hao walikamatwa Julai 8,
mwaka huu katika eneo la Ubungo kituo cha daladala ambapo askari
waliweka mtego wa kuwakamata.
Kamanda Mlege alisema
baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao walipopekuliwa walikutwa na simu
na bunduki aina ya Shot Gun ikiwa na risasi moja, kompyuta mpakato mbili
Toshiba, simu ya mkononi Samsung C3230, panga pamoja na nyundo.
Alisema
baada ya kuhojiwa , inadaiwa walikiri kuhusika na tukio la
unyang'anganyi kwa kutumia silaha la Juni 21, mwaka huu katika Bweni la
Yombo One na kumjeruhi mwanafunzi huyo kwa risasi tumboni kisha kupora
mali mbalimbali.
"Mbali
na tukio hilo pia wamekiri kuhusika na matukio ya uporaji maeneo ya
Ubungo Darajani, Chuo Kikuu na maeneo mengine, ni wahalifu wazoefu sasa
tunaendelea na upelelezi ili kuwafikisha mahakamani," alisema Kamanda Mlege na kutaja majina ya watuhumiwa hao ambao watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Alisema
watuhumiwa hao walipopekuliwa nyumbani kwao walipatikana na mabegi 16
ya kuhifadhia kompyuta mpakato, flashi diski tatu pamoja na vitu vingine
ikiwemo kitambulisho cha mwanafunzi wa chuo kikuu aitwaye Kapalata
John.
Katika hatua nyingine, Kamanda Mlege alisema
katika tukio jingine, polisi walifanikiwa kukamata bunduki mbili aina
ya Shot Gun na bastola tano ambapo mbili kati ya hizo zilihusika katika
mauaji katika eneo la Mbezi NHC.
Bunduki hizo zina namba TZ CAR 59215 ikiwa na risasi nane na tatu zikiwa kwenye kasha la sigara; Nyingine ni yenye namba TZ CAR 79516 ikiwa na risasi tatu zikiwa zimetekelezwa jalalani.
Alisema baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika watuhumiwa Michael Paschal (35), Donald Joseph (43), Kulwa Adamson (43), Ally Akiri (41) na wenzao watano walirushiana risasi na askari katika eneo la Kunduchi Mtongani.
Baada
ya kufuatiliwa, inadaiwa walikamatwa wakiwa na mapanga saba waliyokuwa
wameyaficha kichakani pembeni mwa mto Nyakasagwe katika eneo la Boko
Dovya.
Imeandikwa na Katuma Masamba via HabariLeo
MAJAMBAZI WALIOMJERUHI NA KUMPORA MWANACHUO UDSM YAKAMATWA
0
July 21, 2013
Tags