Majuzi tulisikia mgogoro kati ya kituo cha Television cha Star na
Kampuni ya Startime na tishio la Startv kujitoa. Wizara na Tume ya
mawasiliano wakaingilia kati na kuwalazimisha Startv wapitishe matangazo
yao Startimes ili kukidhi kigezo cha kampuni zenye ving'amuzi kurusha
matangazo ya Bure ya vituo vitano kitaifa ambvyo ni TBC1, ITV,STAR
TV,CHANNEL 10 na CHANNEL 5.
Ajabu ni kuwa mbona jambo hilo limeshindikana kwa DSTV? Mwenye kutumia
kutumia kingamuzi cha kampuni ya Multichoice (DSTV) ni lazima uwe na
kingamuzi kingine maana kama fedha imekata DSTV HUWEZI pata matangazo ya
hizo channel za bure bila malipo.
Je, wizara yako na tume ya mawasiliano mumewashindwa hao wawekezaji?
Maana kama suala hilo kwao halipo mbona channel za kichina zinaonyeshwa
bure?
Hii inamaanisha serikali yetu ina katabia ka kuwaogopa wawekezaji bila kujali maslahi ya wananchi wao?
Fanya utafiti kabla ya kupost usije ukapost pumba. Dstv na Zuku wamesajiliwa na TCRA kama Pay tv. Hawana kibali cha kurusha local channels bure cos hata wao wananunua. Zuku wanadai wanafuatilia kupata leseni lakini hawafungwi na sheria.
ReplyDelete