MANDELA APUMULIA MASHINE..MADAKTARI WAPANGA KUIZIMA


MADAKTARI wanaomtibu Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, wanakubali kuwa kiongozi huyo basi tena kwani hali yake ni tata na sasa wanasubiri kiungo kimojawapo cha mwili wake kishindwe kufanya kazi ndipo wazime mashine inayomsaidia kupumua.

Kutokana na subira hiyo madaktari hao sasa wamebadili msimamo wao wa awali wa kuiondoa mashine hiyo inayomsaidia kupumua.
“Madaktari hao, wameishauri familia yake kuachana na ushauri wa awali wa kuiondoa mashine hiyo hadi tu pale moja ya kiungo chake muhimu cha mwili kitakaposhindwa kufanya kazi,” alisema rafiki wa Mandela, Denis Goldberg ambaye alikuwa mpigania uhuru aliyewahi kufungwa pamoja na Mandela.
Amesema madaktari hao waligusia kuhusu suala la kuondoa mashine lakini baadaye walikataa kwa kuwa kiongozi huyo aliweza kusogeza baadhi ya viungo na kutambua sauti.
“Ni kweli kuwa hali ya Mandela ni mbaya lakini si kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika,” alisema Goldberg.
Juzi vyombo vya habari vya hapa nchini vilitoa hati ya kiapo ya mahakama, ikionyesha kuwa madaktari hao waliishauri familia ya Mandela kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua kwani asingeweza kuendelea kuishi.
Hata hivyo, msemaji wa Rais Jacob Zuma,Mac Maharaj alikataa kuzungumzia kuhusu hati ya mahakama ambayo ilieleza kuwa Mandela mwenye miaka 94 yupo mahututi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad