BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizokamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.
Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania.
Shekiondo alisema dawa walizokamatwa nazo hazitumiki moja kwa moja kama dawa, bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya hivyo kwa mujibu wa sheria, adhabu zao zinakwenda sambamba na waliokamtwa na dawa za kulevya.
"Dawa hizo hazitumiki moja kwa moja bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, hivyo kama taarifa tulizopata ni sahihi juu ya aina ya dawa walizokamatwa nazo na dawa hizi hazitumiki sana nchini, bali zinatumika Afrika Kusini, Asia pamoja na Ulaya," alisema Shekiondo.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.
Akielezea kuhusu wasichana hao wawili kupanda kizimbana juzi, Kamishina huyo aliweka wazi kuwa hadi sasa hawajapata taarifa zozote rasmi, zaidi ya kupokea zile za awali za kushikiriwa na Jeshi la Polisi Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi.
Kamishina huyo alisema inaonesha Watanzania wengi wamekamatwa na dawa za kulevya nchini Brazil ambao idadi yao inafikia 109, ambapo wengi wao wameshahukumiwa.
Alisema watu hao wamekamtwa nchini humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa ajili ya kusafirisha nchi nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa kunyongwa pamoja na kifungo cha maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao bado haijafika rasmi.
"Tumepokea taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa nchini Brazil, ingawa bado tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa kifo, pamoja na kifungo cha maisha," alisema Shekiondo.
Aliongezea kuwa baadhi ya nchi nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa hizo za kulevya wakiwa wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30, Pakistani 16, Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai 14, pamoja na nchi nyingine kama Japan, Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja na Uingereza.
Akizungumzia hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya nchi walizokamatwa Watanzania hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo ndiyo Watanzania wengi wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa Kenya tayari wapo waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo waliohukumiwa kifo na kifungo cha maisha.
Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.
Alisema kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli, jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.
MAPYA YAIBUKA KUHUSU AGNESS MASOGANGE ALIYE KAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA
5
July 18, 2013
Tags
Jamani mpunguzieni adhabu dada masoga
ReplyDeletenge sote tunajua alikuwa kazini,mungu awajalie maamuzi ya busara juu ya hukumu muitoayo kwa masogange.
wacha vijana wahustle wamake kama uongozi unabana hakuna ajira hata mazingira ya ajira tu watu wajiajiri magum, na istoshe nani mwenye uwezo wa kununua na kufanya bisness ya madawa kama sio wakubwaa? msiwalaum hawa watu mazee liangalieni hili swala kwa jicho la tatu
ReplyDeleteHawa ni punda tuu (wabebeshwaji),,,, kuna wakubwa mbele yao
ReplyDeleteThat true ''Punda''wazee wenyewe wametuliya Bila wasiwasi Mapunda wako kibao Bongo.Ukweli matatizo yapo Bongo.Kwanza fix ulanguzi Airport za Bongo.Hao wanaobeba Unga wanapita hapo hapo Tanzania kwahiyo matatizo yako hapo Airport.
DeleteKamishna shekiondo mbona tanzania mnakamata madawa mengi sana hapo airport na mnajisifia mmeweza kuwabana hao wanaosafirisha mpaka kwenye ma tv mnaonesha lakini hatuoni hukumu zao mnasoma hukumu za nchi zingine tuuuuuu jeee zenu hapa bongo au akina nzowa wanauza mzigo hebu mwone aibu NI MIZIGO MINGAPI IMEKAMATWA HAPA NA NINI HATMA YAKE
ReplyDelete