MASKINI WATOTO HAWA WANAUZWA

Na  Juma Kapipi, Tabora
MAHAKAMA ya Mkoa wa Tabora imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya shilingi laki moja (100,000/=) raia wa Burundi, Emmanuel John (22) kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Hivi karibuni, Maafisa wa Idara ya Uhamiaji mkoani hapo walimkamata Emmanuel kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria akiwa na watoto sita aliotaka kuwauza shilingi 1,000,000 kila mmoja.
Mbele ya Hakimu Mkazi Jackton Rushwela,  kijana huyo alikiri kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria lakini alikana kosa la kuingiza watoto kwa nia ya kuwauza.
Kutokana na kukiri kosa la kwanza, Hakimu Rushwela alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya shilingi laki moja.
Kuhusu shitaka la kusafirisha binadamu, upande wa mashitaka ulidai mshitakiwa alikamatwa akiwasafirisha watoto Ndayisenga Batiliza (13), Ndakusenga Emmanuel (15), Nimbonajile Nagenda (13), Yazid John (15), James Justus (14) na Samson Banteke(17).
Baadhi ya watoto hao walitoa ushahidi mahakamani kwamba walisafirishwa na mshitakiwa Emmanuel John kutoka Burundi na Rwanda hadi walipokamatwa eneo  la  Ulyankulu  wilayani Kaliua mkoani hapa.
Kesi ya kutaka kuwauza watoto imeahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu itakaposikilizwa tena kwa mashahidi wengine kutoa ushahidi wao.


Source:GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad