MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22),
amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na
mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto
huo nao walijeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo
lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya
Nzughuni.
Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu
alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha
Nanenane na kisha kujilipua.
“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.
“Watu
waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini
hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na
kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa
karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi,
hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa
kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11)
Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau
(30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).
Majeruhi wote
wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya
hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
Mamae..huyo ni kumtandika viboko hata kama amekufa
ReplyDeletekujiua kwa sisi vijana wengi nw days inatokana na sababu nyingi ila chache ni vijana wengi kutojua wanachokitaka kwenye maisha yao simply lack of focus na kutokumcha mungu plus kukosa shule kichwani..
ReplyDeleteKukimbilia mambo yasiyomuhusu. Uliona wap elimu na mapenzi. Asijali uko kuzim atalipuliwa sana na iyo Petro liya.
ReplyDelete