Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya
Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani alifanya
jambo kubwa muhimu kwa mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata
fursa adhimu ya kufanya mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya
Marekani walioambatana na Rais Barack Obama.
Mpaka sasa kilichozungumzwa na Kiongozi huyo anayeongoza chama
kinachopendwa na watanzania wengi zaidi hakijawekwa bayana ingawa
wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa mazungumzo nyeti na muhimu kwa
mustakabali wa demokrasia na amani ya Tanzania.
Taarifa zaidi zinasema Kiongozi huyo wa Upinzani nchini alialikwa na
Ikulu kwa shinikizo kubwa kutoka ubalozi wa Marekani kutokana na Taifa
hilo kutambua kazi kubwa inayofanywa na wabunge wa CHADEMA ndani ya
bunge la Tanzania.
MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI
0
July 07, 2013
Tags