MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu



"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:


 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huyo.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli aache kujitapa unga unauza unauza na Demu Wako mbona umumejengea Lani hadi kwao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Za mwizi zimetimia,kama vp na yy awataje wenzie.

      Delete
  2. Majina yao ni wafungwa na boss wao ni wewe azzan, subiri sheria ichukue mkondo wake utanyoosha maelezo tu!

    ReplyDelete
  3. Acha paparaa polisi unafuata nini baba sbr watu wafanye kazi yao mnaharibu xana maishaya watanzania wenzenu na kesho kwa allah mnalakujibu.

    ReplyDelete
  4. serikali yote kaishikilia mikononi huyo. anajipeleka tu kutuzuga. hamana hata atakayekamatwa huu ni upepo sasa hivi utapita kama wa richmond

    ReplyDelete
  5. huo ndio mchezo wao,na wapo wengi had jk yupo lkn hawawezi kufanya kitu coz sheria ndio wao wenyewe ila mwisho wao upo njian

    ReplyDelete
  6. Pumbafu mkubwa wew ndio unachangia kumaliza vijana kwa madawa

    ReplyDelete
  7. mshenzi mkubwa unaangamiza taifa,lisemwalo lipo hatakama hujapatikana na hatia ukweli unabaki palepale.

    ReplyDelete
  8. Mwisho wako Qafil mkubwa weeewe

    ReplyDelete
  9. until proven guilty people.. lets wait..

    ReplyDelete
  10. Drugs,credit cards na upigaji mwingine umefanya,wondering hw u got huo ubunge!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad