MJUKUU WA MANDELA AFICHUA 'UCHAFU' WA FAMILIA YAO

Mjukuu wa mzee Mandela...Mandla Mandela alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kijijini Mvezo jana.

Chuki miongoni mwa familia ya Nelson Mandela imeongezeka na kuchukua sura mpya jana pale mjukuu wa kiume na mrithi Mandla kuwatuhumu ndugu zake kwa uzinzi na kuukamua umaarufu wa kiongozi huyo anayeheshimika wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Maoni yake hayo yamekuja wakati mabaki ya miili ya watoto watatu wa kiongozi huyo mwenye miaka 94 ikizikwa upya kwenye eneo la makaburi ya awali kufuatia amri ya mahakama kuirejesha baada ya Mandla kuwa amehamisha miili hiyo.

Katika mkutano na vyombo vya habari uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ambao umewafadhaisha wananchi wa Afrika Kusini, Mandla alithibitisha tetesi kwamba mtoto wake mdogo wa kiume, Zanethemba, alikuwa ni mtoto wa uhusiano haramu kati ya kaka yake Mbuso na mke wa Mandla ambaye sasa wametengana, Anais Grimaud.

Huku Mandela akiwa kwenye mashine ya kupumulia hospitalini mjini Pretoria, chuki hiyo inayoongezeka imeiduwaza na kuishitua Afrika Kusini kwa uwiano sawa.

"Mbuso alimpa ujauzito mke wangu," alisema Mandla huko Mvezo, kijiji kilichoko Eastern Cape kilomita 700 (maili 450) kusini mwa Johannesburg ambako Mandela alizaliwa na mahali ambako Mandla anatumikia akiwa kama chifu rasmi wa ukoo huo.

Mandla, mwenye miaka 39, kwanza aliibua maswali kuhusu ubaba wa mtoto wake mwaka jana wakati alipotengana na Grimaud anayezungumza Kifaransa, ambaye tangu wakati huo alirejea kwao katika kisiwa cha Reunion kilichoko kwenye Bahari ya Hindi. Pia alibainisha wakati huo kwamba hakuwa na uwezo wa kupata watoto.

Juhudi zake kuipata familia hiyo kujibu maswali hayo ya ubaba wa Zanethemba yaligonga mwamba kwa lengo la kuhifadhi mfanano wa umoja katika familia hiyo maarufu kabisa nchini Afrika Kusini," alisema Mandla.

"Jambo hili halikuwahi kabisa kujadiliwa na wanaoitwa ndugu wa familia hiyo ambao wanasema kwamba wanataka kuhakikisha kwamba kuna utulivu katika familia hii," alisema, akiwapa changamoto waandishi wa habari kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha madai yake hayo.

"Ukweli uko pale. Unaweza kwenda na kubaini, fanya vipimo vya muhimu vinavyohitajika," alisema. Kaka yake Mbuso amekana kuwa baba wa mtoto huyo.

Vyombo vya habari vimepachika vichwa vya habari 'Mandela vs Mandela' kwenye kurasa zao za mbele na tahariri zimesikitikia ukatili wa mgawanyiko wa chuki ndani ya familia hiyo ya mtu aliyetikisa dunia nzima kama mfano wa mapatano kati ya pande zinazopingana.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh! Waafrica hatubadiliki kamwe, haya mambi yalitakiwa yasuluhishwe wakati yalipotikea. Aibu sasa.

    ReplyDelete
  2. Duh! Waafrica hatubadiliki kamwe, haya mambi yalitakiwa yasuluhishwe wakati yalipotikea. Aibu sasa.

    ReplyDelete
  3. Jamaani haya mambo yako chini chini ambayo yeye na mimi hatuwazi kufahamu. Ukweli ni huu kuna makabila mengine ambayo kama kaka hawezi kuzaa huwa anasaidiwa na ndugu yake sijuwi hili kwa hawa wezetu. kwa maoni yangu naona kuwa kuna kitu kinacho fichwa huyu jamaa anjuwa ila ameumia kushidwa kesi. maana uweje kuanza kuzungumzia sasa. kama ni kweli au uwongo (Mdogo amezaa na mke wa kaka ambaya uchifu utatoka kwake huyu chifu kisiri leo anapinga parapanda wakati amehifadhiwa yeye.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad