Hayo yalibainishwa na daktari wa moyo anayemtibu
shujaa huyo wa Afrika Kusini, kwamba Juni 8, mwaka huu, wakati
akipelekwa hospitali gari lililombeba lilipata hitilafu njiani na
kukwama kwa muda.
Daktari huyo wa moyo anayeheshimika nchini Afrika
Kusini, (jina linahifadhiwa) alisema jana kuwa gari la wagonjwa
lililokuwa likimpeleka Mandela hospitali liliharibika katika njiapanda
ya Gauteng na kusababisha wasubiri gari lingine kwa zaidi ya dakika 45.
“Moyo wake ulisimama kabisa tukiwa ndani ya gari,
ikatubidi tumfufue kwa mashine (resuscitate),” alithibitisha daktari
huyo bingwa.
Ripoti inaeleza kuwa gari hilo la wagonjwa
linalomilikiwa na jeshi, liliharibika wiki tatu zilizopita kati ya
Pretoria na Johanersburg.
Chombo cha habari cha Marekani, CBS kiliripoti
jana kuwa moyo wa Mandela ulisimama kwa dakika kadhaa kabla gari lingine
halijaletwa na kumpeleka Mandela katika hospitali ya Medi-Clinic.
Wakati moyo wa Mandela uliposimama, nje kulikuwa
na baridi kali kiasi cha nyuzi joto sita tu, hali ambayo inaelezwa kuwa
ilichangia kuharibu zaidi mapafu ya Baba wa Taifa la Afrika Kusini.
“Mke wa Mandela, Graca Machel, alikuwa
amechanganyikiwa kwa dakika hizo 40, ambazo tulikuwa tukisubiri gari
lingine,” kilisema chanzo hicho.
Ingawa msemaji wa Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj
alisema kuwa madaktari wamethibitisha kuwa Mandela hakupata madhara
makubwa kutokana na baridi hiyo, madaktari wengi wameonyesha kupingana
naye.
Daktari wa moyo, David Janekelow alisema, kutokana na hali yake, ucheleweshaji wa aina yeyote ile lazima ulisababisha madhara.
“Unahitaji kupata matibabu ya dharura haraka
iwezekanavyo. Kama mtu tayari alikuwa anafufuliwa, ucheleweshaji wa
kumpeleka hospitali lazima ulete madhara,” alisema Janekelow.
Daktari mwingine wa moyo, Richard Nethonde
alisema, Mandela angekufa pale barabarani wakati wanasubiri gari la
wagonjwa liletwe, imekuwa ni kama bahati hakufa.
Wakati huohuo, gazeti la the Sunday Times limeeleza kuwa Graca,
mke wake analala katika chumba kilicho pembeni ya chumba anacholala
Mandela, kwa siku zote, tangu Mandela alazwe.
Wakati huohuo, wakili wa mjukuu wa Mandela, Mandla
Mandela, amesema atafungua mashtaka kwa baadhi ya wanafamilia ya
Mandela kwa kuidanganya mahakama kuhusu hali ya shujaa huyo.
Wakili huyo, Gary Jansen alisema kuwa wanafamilia
hao walipeleka hati yenye maneno ya uongo mahakamani wakieleza kuwa
Mandela yu mahututi, jambo ambalo limekanushwa na Rais, Jacob Zuma
aliyemtembelea juzi.
“Tutapeleka malalamiko ambayo yatatokana na hati
ya kiapo iliyopelekwa mahakamani na wanafamilia 15 wa Mandela, kwa ajili
ya kufukua miili ya watoto wa Mandela,” alisema Jansen.
Wakili huyo alisema kuwa, wanafamilia hao
walipeleka hati hiyo wakiitaka mahakama ichukue uamuzi wa haraka kwani
afya ya Mandela ni mbaya, jambo ambalo ni la uzushi.
“Lazima tufanye uchunguzi wa kutosha kwa sababu mwanasheria wa familia hiyo, ametumia hati ya kiapo vibaya” alisema Jansen.
Wakati hayo yakiendelea, wananchi wengi Afrika
Kusini wanaendelea kukusanyika katika viwanja vilivyopo karibu na
Hospitali alikolazwa Rais Mandela kumuombea ili apate nafuu mapema.
Habari kutoka ndani ya familia ya Mandela
zinaeleza kuwa huenda mgogoro mkubwa zaidi ukaibuka endapo Mandla
atatimiza azima yake ya kufungua kesi nyingine
Kama mimi binafsi cioni ubaya wowote..ila wasubiri hadi shujaa huyo mandela apate afueni nzuri..
ReplyDeleteKisha ndio wakawasilishe hiyo kesi mahakamani..
Kama mimi binafsi cioni ubaya wowote..ila wasubiri hadi shujaa huyo mandela apate afueni nzuri..
ReplyDeleteKisha ndio wakawasilishe hiyo kesi mahakamani..
huyo mzee wawa2 naxhangaa hao wa2 wanvyogombania sehem ya kumzika angali yuko hai..wafanye v2 vya maana sio kumchuria
ReplyDelete