Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria.
Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili.
Jumla
ya magoli 146 yalifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia
katika vitabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi
ya magoli duniani.
Klabu
ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya Akurba kwa mabao 79-0 wakati
timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza Bubayaro magoli
67-0.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria,
Muke Umeh amesema ufisadi na ulaghahi wa kiwango hicho hakiwezi
kukubalika katika soka ya sasa.
Umeh
ametangaza kuwa baada ya mkutano wa kamati hiyo, ilibainika wazi kuwa
vilabu hivyo vina kesi ya kujibu na hivyo vyote vinne vimepigwa marafuku
ya kushiriki katika mecho yoyote, hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kabla
ya mechi hiyo vilabu vya Plateau United Feeders na Police Machine
vilikuwa na alama sawa na vilikuwa vikipania kupandishwa daraja hadi
ligi daraja ya pili.
Feeders
ilipata magoli 72, katika kipindi cha pili ili hali Machine nao
wameripotiwa kufunga magoli 61 katika kipindi cha mechi yao.
Kufuatia
matokeo hayo Plateau ilimaliza ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na
idadi kubwa ya magoli ikifuatwa na timu hiyo ya polisi.
''Tutachunguza sakata hii na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika'' Alisema Ummeh.
Mkurugenzi
wa michezo na mashindano wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini
Nigeria, Dkt. Mohamed Sanusi, amekariri tangazo lililotolewa na
mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kuwa waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na NFF, vilabu vilivyohusika, wachezaji,,
maafisa wa kiufundi wa timu na wasimamizi wa mechi hiyo watakaopatikana
kuhusika kwa njia moja au nyingine, katika kashfa hiyo ambayo imetajwa
kuwa mbaya zaidi katika historia ya soka nchini Nigeria watachukulia
hatua kali za kisheria.
Source:Shafii Dauda