NISAIDIENI JAMANI MUME WANGU ANANITESA NAONA AIBU HATA KUTOKA NJE YA NYUMBA YANGU

... Dada yangu anauzunika sana!

"Nisaidieni mwenzenu jamani, nina watoto wawili, miaka 6 na miaka 4, wote wanasoma.
siku hizi mume wangu amebadilika sana, kiasi kwamba hata ada za watoto wake hatoi, hadi tugombane sana ndio anatoa ada. Mapenzi pia yamekwisha, anafanya mambo ya aibu hadharani huku watu wakiona.
Kuna siku moja alikuwa na wanawake bar, amewanunulia pombe, huku wanamshikashika, dada mmoja akiwa pale bar ananifahamu akanipigia simu niende nikamuone, nikaenda nikajionea, wanavyofanya, (walikuwa wanamtomasatomasa na kunyonyana), wanamshikashika sana kila sehemu za miili yao (na kisses nyingi). Ndipo nikapata fahamu' "ndiyo maana akirudi nyumbani anakuwa hana hamu na mimi"
Basi siku hiyo nilipata ujasiri nikamfuata pale pale, nikawambia jamani, tafuteni nyumba ya wageni, msitie aibu hapa, wale wadada walikimbia, mume wangu nae akaanza kunikimbiza ili anipige huku kashika chupa ya bia mkononi,
nikajificha mahali, nilipoona amerudi bar, nikarudi nyumbani nikachukuwa nguo nikaondoka, nikakaa kwetu mwezi mzima, badaye akaja kuomba msamaha, nilikubali nikarudi nyumbani kwa huyo mme wangu!.

Kwa sasa ujinga na upuuzi ule umeanza tena, nikimweleza atulie, anakuwa mkali na kunifokea, wakati mwingine ananitukana mbele ya watoto wangu,
"mimi naumia sana moyoni ndugu zanguni"
Mimi sina kazi, nikiondoka tu hata watoto hatawasomeshwa tena, sasa nifanyaje jamani.
Niliwahi kufungua biashara ya kutengeneza nyele (salon), akanifanyia fujo na kunifanya nifunge, hataki nifanye chochote kile,
Naomba ushauri mwenzenu, sijielewi kabisa nifanye nini, ukizingatia mtaa mzima tunakoishi wameishajua tabia yake mme wangu, naona hata aibu kutoka ndani ya nyumba."

"by Happy' she is unhappy"
*Ndugu wanaJF tumsaidieni ndugu yetu Furaha hanaraha kwa sasa.

*Yamkini kuna wadau wako kwenye mazingira kama haya ya Happy.

" Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku, kwa watu wanaoteseka kama ndugu yetu alivyosimulia tatizo linalomkabili, ili tuweza kukidhi mahitajio yake na watu wenye matatizo kama haya."

"SOMA , CHANGIA KWA KUTOA HOJA ZA KUSAIDIA NDUGU YETU NA JAMII KWA UJUMLA."

Karibu wote...

Source:Jamii forums
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dada Happy, kwanza pole kwa matatizo unayokumbana nayo na hiyo ni changamoto tu katika maisha ya mwanadamu, siku zote nyota njema uonekana asubuhi, hapo unachotakiwa kufanya ni kuitisha kikao cha pande zote mbili upande wa mumeo na upande wa kwako muongee ili kutatua hilo tatizo coz huyo mumeo hakukuokota njiani, alikufuata kwenye na kama ameshindwa kukuhudumia kama mkewe na familia yake basi aende akurudishe kwenu na kwa kuwa ni watoto wake ni lazima sheria imbane awasomeshe hilo wala lisikusumbue akili, hao wasichana wa bar watampa magonjwa afu mwisho wa siku atakuletea na wewe nyumbani, ni bora kujilinda mapema na aibu zaidi utakayoipata pindi tatizo likiwa kubwa..

    ReplyDelete
  2. dah pole kwa matatzo

    ReplyDelete
  3. pole sana Dada una moyo wa ujasiri na uvumilivu yote ni mitihani ya dunia stahamili fanya ibada muombee mwenye kusubiri hachoki endelea kusubiri atakulipa mungu hiyo ndio hali ya ndoa ktk majumba yetu

    ReplyDelete
  4. Nitafute namba hii niksaidie kwa mawazo 0715 951095

    ReplyDelete
  5. Pole sana dada nakushauri karibu kanisan tabata segerea mwisho hapo ulizia mtu wa boda boda kwa poster joseph uje huombewe mme wako atakaa sawa na utafurahia maisha yako ya ndoa huyo ni shetani tuu

    ReplyDelete
  6. hebu mbadirike jmn dada zng kwann hv mnajidharirisha bn km jamaa haelewi rudi home na ww pia unawazaz na pia una moyo unauma kwa nn udharirike rudo home kajianzishie vijibiashara somesha watoto km jamaa htak mbona atanyooka tu km ana akili timamu????so chukua nafas namin unaweza cku njema na jikaze una haki

    ReplyDelete
  7. Pole sana bibie! Mungu atakujalia yatakwisha!

    ReplyDelete
  8. Pole sana bibie! Mungu atakujalia yatakwisha!

    ReplyDelete
  9. Pole sana Dada yangu, katika maisha ya ndoa hekima, busara na uvumilivu nimambo ya msingi kuzingatia. Chamsingi waite ndugu wa pande zote mbili ili uwaeleze matatizo yako yote yanayokusibu, wakusaidie. Kwamsaada zaidi nipigie cm no 0766145587. Mungu atakusaidia.

    ReplyDelete
  10. Pole sana kwa yote na uwe na uvumilivu, Kama nyote ni wakristo nenda kwa wazee wa kanisa wamkanye, najua nguvu ya Mungu ni kubwa kuliko zote hapa duniani. Nina imani watamrekebisha tu

    ReplyDelete
  11. Pole dada waite ndugu ya mumeo, na wa kwako mkaa pamoja eleza machungu yako mbele yao, eleza madhara kifikia apo ulipo walio wapata, eleza mipango mliokuwa mmumpanga, eleza mipango livyo kwama kwa sababu ya tabia alioaza, eleza aibu unayo ipata, eleza unavyo mpa na uombe mkutato kusema kama ancho kipata inje amekikosa ndani, kama amekikosa nini? Sema unavyo mpenda mume wako na kuongeza kuwa labda kumpenda kwangu ndiko kumetufikisha hapa mimi nionekane mjinga ukijieleza hayo yote machungu wachie wazee waseme, kama mnasali kanisa fulani mealikeni muchungaji ikiwezekana.

    ReplyDelete
  12. eeeeeh, ndoa pole....., kwanini mnalazimisha watu kuvumilia kwa kiasi hiki, yote anayomfanyia bado mnataka avumilie kisa ndoa, mi sikushauri kuvumili utakufa kwa presha na hao watoto utawaacha watateseka sana, tafuta ufumbuzi wa kutunza watoto wako tafuta kazi karne hii si mwanamke kutegemea mme kwa kila kitu je akifa kesho hao watoto utawafanyaje, acha kujifungia ndani eti aibu toka jichanganye na wenzio upate mawazo ya nini cha kufanya? ili usaidie watoto wako. Pia inawezekana anakunyanyasa kwa sababu anajua unamtegemea kwa kila kitu, huwezi kuondoka kwani bila yeye hujiwezi kimaisha. MWANAMKE AMKA OTHERWISE WANAUME WATATUNYANYASA SANA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad