Anakwambia safari yake ya kutembea kwa mguu kutoka 87.8 Mbeya mpaka
Dar es salaam anaiita Uzalendo Tour kuisupport Taifa Stars na anategemea
baada ya kuimaliza, watu wengi wataiunga mkono timu ya taifa Taifa
Stars.
Anavyotembea kwa sasa anakutana na watu wengi sana na watu wengi
wamekua wakimpigia simu baada ya namba yake kutajwa hewani Clouds FM,
wengine amekutana nao njiani na wamekua wakimpa vitu mbalimbali vikiwemo
viatu na nguo mpya.
Katoka Mbeya saa kumi alfajiri akafika Makambako saa moja na dakika
19 akiwa tayari katembea kilometa 186, akachukua gari mpaka 92.9 Iringa
mjini kwa sababu ilikua imeshakua usiku tayari… akachukuliwa na gari la
Wambura mdau wa Power Breakfast ya Clouds FM na kumuacha Iringa mjini
alikolala mpaka asubuhi na kuianza safari tena.
Anakwambia saa nane kamili alikua anauanza mlima Kitonga na
akaumaliza kwenye saa tisa na dakika kadhaa, baada ya hapo alitembea
mpaka kitongoji cha mwisho kabla ya kuianza Ruaha kisha akachukua gari
mpaka Morogoro mjini kwa sababu ilikua usiku tayari, ameamkia 88.5
Morogoro mjini na sasa anakuja 88.5 Dar es salaam.
Anasema hii ni idea aliyokua nayo kwa muda mrefu sana lakini
akashindwa kuifanya kutokana na kukosa mda ila anamshukuru sana Gerald
Hando wa Power Breakfast @Cloudsfm ambae amemsaidia sana kufanikisha hii
safari.
Sio sehemu zote anatembea kwa mguu, usiku ukiingia inamlazimu apande gari.
Source:Millard Ayo
PICHA ZA MTANZANIA ANAYE TEMBEA KWA MGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR
4
July 12, 2013
Tags
Safi sana!!! Vijana kama hawa wanahitaji kusapotiwa.anastahili kupewa tuzo nakuwekwa ktk record za mashujaa
ReplyDeletewewe jembee!!
ReplyDeleteMbona sielewi,kama kaamua kutembea kwa nini apande gari?
ReplyDeleteAlitakiwa atembee kwa mguu kweli na asipande gari hapo danganya toto
ReplyDelete