Nikiwa kama mtanzania mpenda Haki na Amani ninahuzunishwa sana na
taarifa za kukamatwa, kutekwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa askari wetu wa
JWTZ waliopo sehemu mbalimbali duniani wakipigana vita visivyotuhusu
sisi watanzania moja kwa moja.
Ni huzuni kubwa sana kuona vijana wetu wa kitanzania waliopo jeshini
kutumika kama chambo vitani katika nchi nyingine. Tanzania tusijifanye
ni wazalendo wa nchi zingine wakati wenye nchi zao wenyewe hawazijali.
Zipo namna nyingi bora zaidi za kuleta amani duniani kuliko kupeleka
majeshi ya kupigana vita.
Mpaka sasa bado sijaona faida ya moja kwa moja kwa nchi yangu katika vita hivyo.
Tanzania kwa sasa imepeleka vikosi vyake katika nchi za DRC, Sudan nk.
Ninatoa ombi kwa serikali ya Tanzania kuwarudisha haraka askari wetu
nyumbani waje kulinda mipaka yetu, misitu yetu, Tembo wetu, Makazi yetu,
Mali zetu na maisha ya watanzania. Popote pale mtanzania mpenda Haki na
Amani tuungane katika hili katika kupiga kelele na kushinikiza.
Source:Jamii Forums
TANZANIA TURUDISHE MAJESHI YETU NYUMBANI-TUNATUMIKA KAMA CHAMBO KWA VITA ZISIZO TUHUSU
5
July 21, 2013
Tags
Kuna mambo namaamuz yanayofanywa naviongoz wetu YANAUMIZA sn!!! Cjui wanatuchukuliaje?!?! R.I.P Mwalim Nyerere. 4me tutaheshmiana next uchaguz.. yanini kulazimisha kulalia godoro lenyrkunguni na jamvi lipo?!?.....dawa yenu tunayo.....
ReplyDeleteSamahani mtoa mada ila nadhani kwa hilo unalosema ni sawa na kujitoa ndani ya umoja wa mataifa je ikitokea mapigano tanzania ina maana misaada isije usiongee kwa kufata hisia zako kifo ni sehemu ya maisha na serikali ya tanzania haijipeleki yenyewe bali inaambiwa na umoja wa mataifa msilete siasa jamani kwa kila jambo nchi ngapi zinatoa majeshi yao kusaidia wengine wacha siasa za vibarazani ndugu yangu
ReplyDeleteNingependelea serekali ikapeleka wanjeshi zaidi .kwani hiyo ndiyo kazi waliyo ajiriwa
ReplyDeleteHawana cha kufanya mitaani zaidi ya kunyanyasa raia, waache wakafanye kazi yao si kulipwa bure na kupiga raia ovyo.
ReplyDeleteUsichokijua sawa na usiku wa giza uliza ni kwanini mpango huo upo duniani sio Tanzania tu..TUMEPOTEZA NDUGU ZETU WAKIWA WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO...Africa inatakiwa tuache kujitenga na kujiiona sisi au wale ni bora zaidi au wale waathirka wa kivita ni wajinga... wangekufa wazungu kule mngesema wamefuata nini wachonganishi n.k. Africa itakombolewa na mwafrika tu...
ReplyDelete