Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 109 baada ya
kuifunga Morocco 3-1 mwezi Machi, lakini katika michezo miwili ya kusaka
kufuzu kwa Kombe la
Dunia 2014 iliyofanyika Juni, Stars ilipoteza yote kwa kufungwa 2-1 na Morocco kabla ya kufungwa 4-2 na Ivory Coast.
Wapinzani wa Tanzania CHAN, Uganda wamepanda hadi
nafasi 80, Ethiopia (95), Burundi (120), huku Kenya (123), Rwanda na
Sudan zimefungana 134.
Brazil sasa iko nafasi ya 9 baada ya kutwaa
ubingwa wa Kombe la Mabara na Hispania ikibaki nafasi ya kwanza. England
ikiondoka katika kumi bora na kuangukia nafasi ya 15. Ivory Coast
inaongoza Afrika ikiwa nafasi ya 13,
wakifuatiwa na Ghana (24), Mali (28), mabingwa wa Afrika Nigeria (35)na Zambia (60).
Mabingwa wa Oceania, Tahiti wameshuka kwa nafasi
16, kutoka 138 hadi 154, baada ya kufungwa mechi zote tatu za Kombe la
Mabara kwa jumla ya mabao 24.