TANZANIA YAPOROMOKA KIMPIRA VIWANGO VYA FIFA

Kipigo ilichokipata Taifa Stars kutoka kwa Morocco na Ivory Coast imeishusha Tanzania kwa nafasi 12 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa) kutoka nafasi ya 109 hadi 121.
Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 109 baada ya kuifunga Morocco 3-1 mwezi Machi, lakini katika michezo miwili ya kusaka kufuzu kwa Kombe la
Dunia 2014 iliyofanyika Juni, Stars ilipoteza yote kwa kufungwa 2-1 na Morocco kabla ya kufungwa 4-2 na Ivory Coast.
Wapinzani wa Tanzania CHAN, Uganda wamepanda hadi nafasi 80,  Ethiopia (95), Burundi (120), huku Kenya (123), Rwanda na Sudan zimefungana 134.
Brazil sasa iko nafasi ya 9 baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mabara na Hispania ikibaki nafasi ya kwanza. England ikiondoka katika kumi bora na kuangukia nafasi ya 15.  Ivory Coast inaongoza Afrika ikiwa nafasi ya 13,
wakifuatiwa na Ghana (24),  Mali (28), mabingwa wa Afrika Nigeria (35)na Zambia (60).
Mabingwa wa Oceania, Tahiti wameshuka kwa nafasi 16, kutoka 138 hadi 154, baada ya kufungwa mechi zote tatu za Kombe la Mabara kwa jumla ya mabao 24.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad