Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari
hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la
kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen
Ulimboka.
Mwandishi
wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi
alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi
huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha
amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba
kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha
kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo
mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema
kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za
binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na
ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na
mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.
Aliongeza
kuwa Julai mwaka jana, serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la
kila wiki la Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu
tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu
huo na serikali ya Rais Kikwete.
Kamati
ya Kulinda Waandishi wa Habari yenye makao makuu yake New York nchini
Marekani, wiki jana ilimtaka Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa
vyombo vya habari atakapokutana na Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na
ambayo haikutegemewa wakati bomu la kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa
katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa
CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.
Source:http://www.nytimes.com/2013/07/01/world/africa/violent-episodes-grow-in-tanzania-an-african-haven.html?_r=0
TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI
4
July 02, 2013
Tags
dah kweli vijana mmeongea sana.ila inaonekana hao wenye silaha na wenye kuichafua serikali mnawajua sasa si muwataje tu jamani.maana naona mnapindisha maneno hapo juu
ReplyDeleteUnafiki wa serikali ya ccm unafikia ukingoni.Kujaribu kuzuia nguvu ya ya umma ya mageuzi ni sawa na wendawazimu wa kuzuia mafuriko kwa mikono.Hongera New York Times!
ReplyDeleteBreaking News,Serikali ya ccm,kupitia kwa waziri wake wa habari George Mkuchika imelifungia gazeti la NewYork Times milele.Gazeti hilo linatuhumiwa kwa kuichana live serikali na kuandika jinsi mikono yake ilivyochafuka damu za raia wake iliyowaua. Mhariri .
ReplyDeleteDun!New York Times na Mwanahalisi ni dugu moja.
ReplyDelete