SERIKALI ya Tanzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka
isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo
kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza.
Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya
Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali
yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya
Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa
wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa
inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile
alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.
Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa
kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30,
nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.
Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika
baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi
ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao
na kumchapa.
Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana
waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na
kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia
akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri
majadiliano….majadiliano?”
Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo
hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’.
“Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali
hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga
kumtisha Rais Kikwete.
Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda
wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya;
“Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.”
Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya
kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais
Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi
za Maziwa Makuu.
Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo
ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro
inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na
jumuiya ya kimataifa na SADC.
“Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo
kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema
Mkumbwa.
Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama
kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake.
Chanzo cha mzozo
Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya
kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho
kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini
ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa
wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa
alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda
zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya
vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC.
Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni
akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”.
Hata hivyo, matamshi
hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa
tamko bungeni.
Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma
hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta
mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi.
Akaongeza
kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na
wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini
na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa
busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli,
dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete.
Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya
kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema
Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa
Rwanda pia kufanya hivyo.
“Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno
ya nini tena? Hutaki ushauri basi.
Maneno ya kila siku ya nini? Tangu
Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma
Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili
ya nini?
“Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994
na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri
mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu
wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na
wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,”
alisema Zitto.
Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili
zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu
wake na si vita ya mtutu wa bunduki.
“Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka
pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana
yoyote,” alisema.
Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia
zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na
mikoa ya mpakani ya Rwanda.
“Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima
harakati za kujenga demokrasia nchini. Busara itumike tu,” alisema
Zitto.
Tanzania Daima
Kikwete anazuga tu na kujaribu bila mafanikio kuhamisha mjadala wa kitaifa na hali mbaya ya amani aliyoivuruga hapa tanzania kwa mikono yake mwenyewe inayonuka damu.Utaweza je kumshauri Kagame kabla ya kutatua matatizo ya tanzania ambako polisi,ccm na usalama wa taifa wanateka,kutesa,kung'oa meno,kunyofoa kucha na kuua raia? Kikwete anapenda sana political musterbation!
ReplyDeleteKikwete ni kama demu tu kwa kidume rijali Kagame.Kagame ,usiache kumpiga miti kikwete akiingia kwenye kumi na nane zako!
ReplyDeleteANONYMOUS KIKWETE NI KAMA DEMU WEWE MWENYEWE NI DEMU SIO KAMA SO ACHA UJINGA WEWE MBULULA WA FIKRA FISI MAJI.
Deleteinchi ya siasa kali baba tanzania inaitwa chokoza ukawone. mtakipata cha mtemakuni
ReplyDeleteBig-up Kikwete nashangaa hawa mang'ombe wanaokuponda wakati wao hawawezi kuteuliwa hata kuwa balozi wa nyumba kumi, watabaki domo tu but nothing they know
ReplyDeletevita haina faida,tusubli tuchokozwe mkuu,pili mtu mpumbavu mlekebishe bla ugonv,naye atakushukulu
ReplyDeleteKwanini tunagishukuu? Kagame hajamtajaa mtuu...amesema about those one who surpport interahamwee Atapambana nao...is Kikwete among them?? If he is not among them,why do you have borther?? Si Rais wetu hausiki na nterahamwe...then why are we shauting at Kagame?

ReplyDeletekagame akiyakanyaga anyooshwe tu, tumeshachoka mikwara, vijinch vdg vdg kama mikoa, pambafuuuuuuuuu........!
ReplyDeleteTry Kagame and see the secret in his small country of his....God can't give big country and the power.mbinu za vita vip??? au ni makelele tuu?

ReplyDeleteNyie mmbwa mnao mponda raisi kikwete wekeni maslai ya taifa mbele nasio kubeza kila chenye mafanikio. Nyie mlitaka raisi wa nchi hii awe baba yenu?msilete siasa kwenye jambo hili.
ReplyDeleteFor the sake of the citizens of both countries ,Kagame and Kikwete they won't fight and they will never fight ok. Brothers don't fight they just get miss understings! Who will allow them to fight???? Lukuusa kawapaaa nani??? Ebu ingueni DRC mkaibe madini ni mengi sanaaa bado.
ReplyDelete