Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.
Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa
na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi
kabisa.
Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi,
wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta
wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.
Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na
kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma
zao.
Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa
wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili
kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani
lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.
Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi
imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu
kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani
badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?
Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana
kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu
wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…
Tunaomba statistical data juu ya hili
ReplyDeleteAchunguze labda Mkewe ni Msagaji na anafanya hvyo na house girl, then atafakari achukue hatua.
ReplyDeleteKweli nfumo ya elimu wetu sio mzuri tumesikia wanasiasa wanasema eti kila somo kuazia shule ya msingi hadi chuo kikuu iwe ni kishwahili. Huo ni uongo mkubwa sana tena sana hao wanaosema toto wao wanasoma India, Malasia, USA, Ulaya nk. wanasema mbona wezetu wa china wana jiweza. uongo mtupu mchina anajiweza haitaji msaada kutoka sahemu yoyote kama sisi. Angelikuwa ni nyerere ningalisema acho kisema tufanya kitafanyika hata kwa watoto wake. Ila kwa wanasiahasa wetu wata weka watoto wetu katika shule hizo wakati wa kwao wameluka na mapipa tusidanganywe waTZ
ReplyDelete