Ndoto ya wasichana wengi ni siku moja kuja kuolewa. Mungu ametuahidi
baraka zake nyingi ikiwamo baraka ya ndoa hivyo haupaswi kukaa na
kusubiri hadi upate mchumba ndio uanze maandalizi yakupasa kuanza
kujiandaa kuwa mke. Mungu amekuandalia mume mwema hivyo unapaswa
kujiandaa mapema ili ndoa yako iwe bora.
1. Omba kwa ajili ya mume wako Wasichana wengi wanaomba ili waweze
kuolewa, hiyo ni sawa kabisa lakini jambo la kwanza kabisa inabidi uombe
kwa ajili ya mume wako ambaye Mungu anaenda kukupatia. Anza mapema
kuomba kwa ajili ya mume ambaye Mungu anaenda kukupatia. Omba kwa ajili
ya maisha yake ya kiroho, uwezo wake kusimamia na kuitunza familia na
maisha yake kwa ujumla. Usisubiri hadi uolewe ndipo uanze kuombea umoja
katika ndoa yenu, anza sasa na pia kumbuka kuomba kwa ajili yako ili uwe
mke mwema.
2. Jiandae Familia yako unayoishi nayo ndio hasa sehemu yako ya
kujiandaa kuishi na mume wako. Unapaswa kujifunza kuanzia sasa kuishi
vizuri na watu wa familia yako, hutaweza kuishi vizuri na mume wako kama
sasa unashindwa kuishi vizuri na ndugu na jamaa zako. Waonyeshe upendo,
huruma na kujali na kwa kufanya hivi utakuwa umejijengea tabia ambayo
utakuwa nayo kwa watu wote na mumeo pia. Unaposhindwa kukaa vizuri na
watu wako wa karibu kama familia vivyo hivyo hautaweza kukaa vizuri na
mume wako, ndoa haimbadilishi mtu bali inakuonyesha uhalisia wako. Jinsi
ulivyo unapokuwa nyumbani kwenu ndivyo ulivyo.
3. Omba uweze kutambua hila za shetani Sababu ya uhitaji wa kuolewa
ulionao inaweza kuwa ngumu kugundua kama mtu anayetaka kukuoa hajatoka
kwa Mungu. Sio kila nayesema Bwana asifiwe ni kweli ameokoka maana
wengine wapo ili wapate wake wazuri, ndio maana ni muhimu sana kuomba
uongozi wa Mungu ili uweze kujua nani hasa ametoka kwa Mungu. Pia
inawezekana akawa ameokoka lakini akawa sio mume ambaye Mungu
amekuandalia hivyo ni muhimu sana kuomba kwa ajili ya uongozi wa Mungu
katika muda huu wa muhimu katika maisha yako.
4. Tulia mbele za Mungu Filipi 4:6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote;
lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na
kuomba pamoja na kushukuru Mungu analifahamu hitaji lako na muhimu zaidi
anakujua na kukupenda, hajakusahau maana hawezi kukusahau na anakuwazia
yaliyo mema. Ebrania 13:5b kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita
kupungukia kamwe wala sitakuacha” Yeremia 29:11 Kwa maana ninajua
mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’ asema BWANA. “Ni mipango ya
kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru,ni mipango ya kuwapa tumaini
katika siku zijazo”. Usikate tamaa, mume wako yupo na atakuja kwa wakati
wa Bwana.
Endelea kumwamini Mungu. Ubarikiwe!
Source:Jamii forums
Amen
ReplyDeleteLeo mdau upo on point chukua tano!
ReplyDelete