Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com,
M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47
yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook
ikiambatana na picha hiyo:
“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka
Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko
Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu
zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa
cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya
kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC
ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita,
sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone
passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”
WAASI WA M23 WAWEKA PICHA YA PASSPORT YA MWANAJESHI WA TANZANIA WALIO MTEKA HUKO CONGO
0
July 20, 2013
Tags