Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa
Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue
Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege
kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa
(crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na
zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo
timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika
mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja
katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“When searching their luggage which was six large bags of black
holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal
meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are
valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the
SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.
WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANI
0
July 08, 2013
Tags