ABIRIA WA TANZANIA AKAMATWA HONG KONG NA MADAWA YA KULEVYA YAKIWA NDANI YA MASHINE
1Udaku SpecialAugust 16, 2013
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
sasa hivi hawa wauza sembe watafute biashara nyingine hii ishatumbukia nyongo hailiki tena hii inaitwa zilipendwa mnao ibukia mnajifanya bonge la wajanja kumbe woote mtaenda na maji wacheni mara moja imeshasanuka hata uficheje itakamatwa tu tafuteni kazi ya halali vijana utajiri wa harakaharaka ukufikishi mahali muache tamaa tamaa mbaya fanyeni kazi ya halali Mungu atawabariki mtafanikiwa mkifanya kazi ya halali kwa bidii

ReplyDelete