AIBU: MKE AFUMANIWA AKIGAWA URODA CHUMBANI KWA MUMEWE


Timbwili I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita  na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao..

Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.

Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.


Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.


 Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.

Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo .

  Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.

Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.

 Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.


Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.



Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia. 
 

Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.

Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.


Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
 


Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.

Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.



Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.


Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.

“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.

Source: Global publisher

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna ndoa ya bomani kwa muislam. Sa uyo dada aliolewa au alikua anazini na uyo mnaemuita mumewe. Laana tupu.wote wanazini si mume wala alofumaniwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania(THE LAW OF MARRIAGE ACT [CAP 29 R.E. 2002])haina sehemu ambayo ina mlazimisha/kumshurutisha mtu wapi pa kufungia ndoa- ni mapenzi/uamzi wako, so imekupa uhuru wa kwenda kufunga ndoa popote pale pawe mskitini, kanisani au kwa mkuu wa wilaya ambapo wewe unapaita bomani. Kwa huyu muislam si kosa kufunga ndoa ya serikali kwani hawa mashehe, mapadri,wachungaji, wakuu wa jadi,wakuu wa wilaya(tuseme wafungishaji ndoa waliochaguliwa na kutambulika)ni wakara wa serikali katika suala la kufungisha ndoa.

      Delete
  2. hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......jamani huyu rwekaza si mwalimu wetu magogoni? Kha!maadili yamemshinda sisi atatufundishanini?

    ReplyDelete
  3. Nimependa ulivyo elezea kuhusu wapi pa kufungia ndoa kwa mujib wa sharia, je nawezaje kupata nakala ya kitabu hicho cha sharia ya ndoa? @ Anonymous

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad