Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza sio la kigaidi. "matukio haya yasichukuliwe jumla jumla, sisemi moja kwa moja kuwa tukio hilo ni la kigaidi ila naomba tuhamasishe jamii ya watanzania utii wa sheria bila shuruti, na tusaidie vita dhidi ya matumizi mabaya ya tindikali" - Alikuwa anajibu swali kama tukio la Tindikali nalo ni la kigaidi kama yale aliyopitisha ofisini kwake yafunguliwe mashtaka ya Ugaidi yaliyokataliwa na Mahakama
IGP- Amekwepa swali la kuwa endapo yupo tayari kujiuzulu kwani matukio mabaya yamekuwa yakiendelea tu.
"Kwanini usijiuzulu kwa kuwa matukio kama haya yamekuwa yakijirudia, na wewe umekalia kiti hicho?"
Hayo yamejiri kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani muda mchache kulikuwa na Press conference, Wazungumzaji walikuwa ni IGP, DPP na Mkemia Mkuu wamechanganyikiwa na tukio la Waingereza kumwagiwa Tindikali. Pamoja na hayo, hoja yangu je Serikali inaamka wageni wakiguswa? tangu lini matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameanza kutokea na serikali haichukui hatua, wala kukamata watuhumiwa. Mabomu yamelipuka hatujawahi kusikia serikali ikitoa maelezo na namna ya kujilinda. Leo la tindikali la Waingereza IGP, DPP na Mkemia Mkuu wanafika kueleza namna ya kudhibiti tindikali, na namna ya kupata taaarifa za tindikali.
DDP: "TUKIO LA TINDIKALI ZANZIBAR SIO LA UGAIDI"
0
August 10, 2013
Tags