HATIMAYE KESI YA WALE WACHUNGAJI WA DESI YATOLEWA HUKUMU LEO, MMOJA ANUSURIKA

Wachungaji watano wa makanisa ya Kipentekoste waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma kwa kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi Tanzania na kuijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao, Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia na wengine wanne wamehukumiwa kwenda kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.
Kesi hiyo iliyokuwa ikiunguruma mahakama ya Kisutu Jijini Dar karibu miaka mine iliyopita mahakama hiyo kupitia hakimu wake Aloyce Katemana ilitoa hukumu hiyo baada ya kulidhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi na Jamhuri. Waliopanda Desi nao waambiwa wanakesi ya kujibu.
Picha juu ni baadhi ya matukio yaliyojiri mahakamani hapo.
Source:GPL

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao wanyongwe tu na mbegu zetu tulizopanda zimeshaoza mbaka sasa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad