HENRY KILEWO "WATATUDHALILISHA KWA MUDA NA SINTAOGOPA KUKAA JELA NI MUDA TU TUTASHINDA"

Baada ya kutoka jela Henry Kilewo Amesema haya:
"Kwa watanzania wataka mabadiliko: jela siyo sehemu salama ya kuishi,wala haijawahi kuwa sehemu salama ya kuishi,wala haitakaa iwe sehemu salama ya kuishi pasipo tokea wajasiri na wazalendo kama mimi na wewe kwenda kuishi kwa hiari sehemu ambayo utawala dhaifu wa ccm unadhani ni kitisho cha kuzuia mabadiliko. Watawala wabovu kwenye nchi yetu hutumia jela kama kitisho cha kuzuia ukweli,ukiruhusu kitisho cha kuogopa jela utakuwa mwanamabadiliko kigeugeu na mnafiki machoni mwa umma. Kitisho hiki kamwe sintokiruhusu mimi henry kilewo hata kwa mtutu wa risasi za moto,japokuwa natambua athari za kukaa jela muda mrefu kama ambavyo shujaa wa dunia nelson mandela anavyopitia kwasasa, hii kwangu mimi ni sadaka tosha kwa taifa langu chama changu, familia yangu pamoja na ndugu jamaa na marafiki zangu. Nionyo na funzo kwa watawala dhaifu kudhani wataweza kuzuia harakati hizi za mabadiliko kwa kuvitumia vyombo vya dola vibaya kama usalama wa taifa, jeshi la polisi, mahakama na hata magereza. Kamwe tusiruhusu kuwa wanyonge wala kukubali kuonewa kwani watatuzuia kwa muda, watatudhalilisha kwa muda na sikuogopa kukaa jela ila moyo wangu unasononeka pale nionapo saa ya ukombozi inachelewa. Ni muda tu, tutashinda" Says Henry Kilewo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad