Msanii Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.
Ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wfanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini. Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
Akikanusha taarifa hizo Diamond alisema “ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo. Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”
Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.
Source; 24Hours Mix
Msenge tu huyo Ana hela gani tunajua siri zao
ReplyDeleteKITAELEWEKA TU
ReplyDeleteuache mara moja kama ni kweli una damu ya kunguni hutakawia kukamatwa
ReplyDeletezinahitajika evidence zamaana na za kutosha kumhucsha m2 kwe sembe..la cvyo mna mchafua m2 aonekene ndivyo cvyo
ReplyDeleteEti cku zote kazi ngumu ndo zinalipa, ingekuwa hivo makuli,wamwaga zege, c wangetajirika?inaeleweka duniani kote kuwa kaz za magendo ndo zinazo lipa,huyo dogo anatia shaka
ReplyDeleteYaan hata mm nina mashaka nae kama kuimba kuna wenzake wameanza kuimba kabla yake hdi mate yamewakauka haiwezekan yy aanze juz tu awe hivyo cbure kuna namna
ReplyDeletePole sana msanii wangu ila kama no kweli acha maana vijana wanateseka sana jamani
ReplyDeleteAna rahisi kuudanganya uma akae akijuwa wakati umefika ss hawezi kuwa na hela kama hizo hata kama angetambikia kwao, wanauwa wtt wa watu kwa tamaa zao za muda mfupi ameukalia ss.
ReplyDeleteHata kujitetea tu kiakili chenga yy anaona kutamka $ 30,000 ni kitu kidogo sana yy kaenda kutengenezea nyimbo 1 angalie maneno yake yatampoza, kwanza kwa show gani anayofanya mpaka angize kiasi cha yy kjikim alafu na zibaki nyingine nyingi za kutengeneza wimbo kwa gharama hiyo, labda kama kuna mtu ana mpakata kisha anamwonga mshiko mrefu kama huo, ukizingatia yy ana muuziz nani hizo nyimbo zake mpaka amlipe mihela yote hiyo na huyo mtu apati hasara kwa ninavyo wajuwa wabongo siku hizi awanunui cd wala casset yy auza wapi. chezea bwibwi ww.
ReplyDeleteUmeona mansion anayoporomosha mbezo beach?muzoki tu wa kibongo ndio uwe na mahela machafu kiasi hicho?haki ya nani mi Siamini.Kuna namna.
ReplyDeletemmh hata kujitetea hajui aiseee ni noumaah
ReplyDeleteHaters!!!
ReplyDelete