HII NDO KAULI YA KWANZA KUTOKA KWA NDUGU WA AGNES MASOGANGE, KUHUSU NDUGU YAO KUKAMATWA NA MADAWA

 FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli. “Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.

Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.

Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:

TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?

Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.

Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.

Masogange na nduguye, Mellisa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na ‘unga’ kilo 150 aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hicho ndo alichokuwa anakitafuta, wacha makaburu wamfire kwanza.

    ReplyDelete
  2. mmmh we baba ulikuwa wapi kumuombea siku zote kwa mhungu hebu tutolee utumbo hapa

    ReplyDelete
  3. Una laaana we baba,mwanao mpaka anacheza much za uchi ulikuwa wapi?ebu kwendra ukooooo.na ulokole wako.

    ReplyDelete
  4. inaonekana matatizo yote hayo ni radhi za wazazi wako pole sana binti

    ReplyDelete
  5. Mademu wa kibongo tamaa mbaya ,si alikuwa anaweka picha fb ameshika mihela kibao aliona fahari basi atumikie huko ,huyo mzazi mbona hatukuwahi kumsikia ,huenda ndio laana za mzaz zimemfika ,jamani fahae za shortcut zina majanga sana kuweni macho ndugu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad