HUYU NDIO MWAKYEMBE BWANA. ATINGA UWANJA WA NDEGE SAA KUMI ALFAJIRI KUKAGUA MIZIGO!

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, ameanza kufanya ziara ya kushitukiza jana saa 10 alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kuangalia mwenendo mzima wa usafirishaji wa mizigo.
Katika ziara hiyo alitembelea vitengo mbalimbali, kikiwemo cha ukaguzi wa mizigo na abiria pamoja na kitengo cha kamera, ambako hivi karibuni kulipita dawa za kulevya za mabilioni.
Dk Mwakyembe amefanya ziara hiyo siku tatu baada ya kuahidi kuhakikisha inawatia mbaroni watu wanaojihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege, kikiwemo hicho chenye jina la Baba wa Taifa.
Meneja wa Usalama wa wanjani huo, Clemence Jingu, alikiri Dk Mwakyembe kufanya ziara hiyo ya kushitukiza, ambapo alioneshwa maeneo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa uwanjani hapo wakati wa ukaguzi wa mizigo.
Mtoa habari wetu alisema Dk Mwakyembe, alitembelea eneo ambalo dawa za kulevya zilipita na kukamatiwa nchini Afrika Kusini.
Alisema Dk Mwakyembe aliona hali ya ukaguzi katika eneo hilo ilivyokuwa, na kubaini dawa hizo zilionekana katika mizigo lakini kulikuwa na uzembe au njama zilizotokana na maofisa waliokuwa wakikagua.
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Dk Mwakyembe alipita katika eneo hilo, ambalo lilikuwa na ofisa wa Polisi ambapo alielezwa kuwa siku hiyo mbwa wanaotumika kubaini dawa hizo, walicheleweshwa kufika.
Dawa hizo za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.8, zilikamatwa nchini Afrika Kusini hivi karibuni wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka nchini humo, wanawake wawili walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini, wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa wakiwa na mabegi sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na kilo 150 za dawa hizo, ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’.
Akitoa ahadi ya kukabiliana na biashara hiyo wiki hii, Dk Mwakyembe amesema anajitoa mhanga kuhakikisha Wizara yake inawatia mbaroni watu wanaojihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
“Nitajitoa mhanga juu ya biashara hiyo na siogopi vitisho vya watu, maana mimi nilishakufa siku nyingi, hatuwezi kuidhalilisha nchi yetu kiasi hicho.
“Dawa za kulevya sasa zinasafirishwa kupitia kiwanja cha ndege, ambacho kimepewa jina la mtu muhimu katika nchi yetu, Mwalimu Nyerere, ni aibu kwa nchi yetu na Taifa letu, kuona uwanja huo unatumika kwa biashara hiyo, nipeni muda, mimi ndiye Waziri wa Uchukuzi, hatutakubali hali hii,” alisema na kuongeza: “Pale uwanjani kuna ofisi nne, Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, wote nimewaagiza wanipe taarifa, walikuwa wanafanya nini hadi dawa hizo zinapita uwanjani hapo?”
Alisema anawapa notisi watu wote wanaosafirisha dawa za kulevya kupitia uwanjani hapo, watambue kuwa alishajitoa mhanga kupambana na dawa za kulevya, maana ni biashara inayodhalilisha Taifa.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe ndio waziri sasa! tunahitaji watu kama wewe kwenye taifa letu, tunataka vitendo sio blaa blaa kama viongozi wengine. Mungu akusimamie katika utendaji wako wa kazi

    ReplyDelete
  2. Kila kiongozi akiwajibika ipasavyo kwenye nafac yake kama wewe!! Tanzania itakua ulaya sasa hivi!! Big up bro Mwakyembe watanzania tupo nyuma yako na tunajua nani kiranja? Na nani kiongozi!

    ReplyDelete
  3. i love u mwakyembeeeee

    ReplyDelete
  4. Replies
    1. nipe namba yake ntampa umeumia eeeh mbeba unga wewe nyambaffff mtadakwa mwaka huu na jembe langu

      Delete
  5. Uwakamate wote walio kua zam ck ya tukio waweke ndan hadi watoe maelezo ya ktosha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad