KWANINI IKULU IMEKAA KIMYA JUU YA MATATIZO YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI?

Kwa takribani mwezi sasa, taarifa za kuwahusisha watanzania wenzetu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya zimezagaa karibu ulimwenguni kote. Tumesikia watanzania wenzetu wakikamatwa hongkong, zimbambwe, Afrika ya kusini.. na kwingeneko..

Swali nilojiuliza ni kwanini IKULU imekaa kimya sana juu ya matukio haya.. hata kueleza ni hatua gani zitachukuliwa kuinusuru nchi dhidi ya madawa haya... au kunamkaati gani dhidi ya baishara hii inayotuharibia sifa sifa nchi za nje tofauti na maiaka ya 80 na 90 ambapo watanzania tulikuwa tukisifiwa sana nchi za watu..kuwa watanzania ni watu makini na wema sana wasio na mambo maovu ovu kama haya ya madawa ya kulevya. 

SASA KWANINI IKULU IPO KIMYA TU KUHUSU HAYA, WAKATI RAIS ALIAPA KUILINDA KATIBA, NA KUITETEA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WA TU WAKE, AU HII ISHU YA MADAWA YA KULEVYA SI TATIZO KWA IKULU KAMA AMBAVYO SISI WATANZANIA WENGINE TUNAVYOONA?? Tumeona sakata la wahamiaji haramu halijachukua muda tangu RAISI atoe oda ya watu hao kuondoka na tayari watu hao wameshaondoka na tarifa zimetolewa na vyombo vya habari.. Tuliona hata sakata la mpaka kati yetu na malawi.. Ikulu ilikuwa ikitoa taarifa mara kwa mara juu ya uhalali wetu kumiliki sehemu ya ziwa hilo..

KWANINI HILI LA MADAWA YA KULEVYA IKULU IPO KIMYA?? HATA KATIKA HOTUBA ZA RAISI ZA MWISHO WA MWEZI SIJALISIKIA HILI LIKIZUNGUMZWA, WAKATI 2005/2010 JK ANAINGIA MADARAKANI ALISEMA ANAYOMAJINA YA WAFANYA BIASHARA WA MADAWA YA KULEVYA NA ATAYAFANYIA KAZI .. LAKINI TANGU 2005 MPAKA SASA RAISI ANAKARIBIA KUMALIZA MUDA WAKE HAKUNA KITU.. NA BAISHARA NDIO INASHAMILI.

SASA JE KAMA HATUA MADHUBUTI SISIPO CHUKULIWA SISI KAMA RAIA TUNAWEZA KUFANYA LOLOTE JUU YA SERIKALI YETU KUWAJIBIKA?? MAANA SIDHANI KAMA NI SUALA LA KUMWACHIA WAZIRI MMOJA HILI..

TUJADILI KWA MASLAHI NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU TAFADHALI...

Source:Jamii forums
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwasababu ikulu haiwezi kusema

    ReplyDelete
  2. huwenda kuna siri kubwa ndani yake.......!

    ReplyDelete
  3. Hao watoto wa rais wanauza unga na ndio vinara sasa unadhani nani atalizungumzia huko ikulu ,na wametajirikia biasharA hiyo ya madawa ya kulevya ,tunajua kila kitu

    ReplyDelete
  4. Namshangaa rais anpoteza pesa nyingi kwenye sober houses kuliko kuzuia madawa yasiingie nchini kuna siri kubwa hapa

    ReplyDelete
  5. Hivi Freddy na Ridhiwan ni wabunge,sijaka bongo muda sasa,ndio maana mambo ya bongo yananipita.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad