MAJANGA:MUHADHIRI UDSM AUWA KINYAMA DAR , WAZUNGU WAMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR

Mauaji, mashambulizi ya kudhuru mwili na uporaji vimeendelea kuchafua taswira ya Tanzania baada ya juzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao hawajafahamika, raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali na mfanyabiashara kuporwa zaidi ya Sh40 milioni.

Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda Hospitali ya Aga Khan kuwajulia hali raia hao wawili wa Uingereza waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18) akisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.

Mauaji

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema jana kuwa mauaji ya Mhadhiri huyo Msaidizi katika Idara ya Uhandisi na Teknolojia, Patrick Rweyongeza (32) yalitokea juzi saa saba mchana maeneo ya Magomeni Tanesco, Dar es Salaam, wakati marehemu alipokuwa ndani ya gari lake akielekea katikati ya jiji.

“Alipofika maeneo hayo alivamiwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Boxer ambao walimpiga risasi ya kifua upande wa kulia kisha kutokomea.”

“Baada ya kupigwa risasi alipelekwa Muhimbili lakini kabla ya kuanza kupatiwa matibabu alifariki dunia,” alisema Kamanda Wambura.

Alisema hakuna mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. “...Tunaendelea na upelelezi kufahamu tukio hilo lililofanywa na watu hao kama ni la ujambazi au kisasi.”

Akizungumza nyumbani kwa mjomba wa marehemu Mbweni, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Uhandisi, Dk John Mahunza alisema Rweyongeza alikutwa na mkasa huo baada ya kutoka benki kuchukua fedha kwa ajili ya shughuli za ofisi.

“Baada ya kuchukua fedha hizo Ubungo, alipanda gari kuelekea Magomeni na kufika maeneo ya Tanesco, walimzingira na kumlazimisha kufungua mlango, lakini aligoma na wakampiga risasi,” alisema.

“Baada ya kumpiga risasi mkononi, walimpora bahasha iliyokuwa na fedha... nadhani wale walikuwa wanamfuatilia tangu alipokuwa benki hadi anatoka.

Source:Mwananchi

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. la busara na usalama hizo pikipiki zote zingezuiliwa labda uhalifu ungepungua maana sasa hivi hizo pikipiki ndio zinazofanya ujambazi aambiwe RAIS alishughulikie suala la PIKIPIKI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad