Imelda Mtema na Denis Mtima
HATIMAYE mama mzazi wa Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi, amefunguka kuhusu madai kwamba mwanaye amenyongwa nchini Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
Mama huyo aitwaye Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar, amesema kuwa mwanaye amefungwa miaka mitatu na nusu na anawasiliana naye kwa njia ya simu kila baada ya miezi miwili.
“Taarifa za mwanangu kunyongwa si za kweli bali amefungwa miaka mitatu na nusu,” alisema mama huyo.
Mama huyo amemtupia lawama rafiki wa karibu wa Binti Kiziwi aliyemrubuni kufanya biashara hiyo ya kusafirisha madawa ya kulevya.
“Sikuijua safari hiyo ya mwanangu ila nilipigiwa simu na rafiki yake wakiwa wameshafika Nairobi, Kenya,” alisema.
Kama vile haitoshi, mama huyo anamlaumu rafiki kwa kuchukua dola 5,000 za mwanaye alizokutwanazo wakati akikamatwa.
Mbali na kuwasiliana na mwanaye, mama huyo amesema Binti Kiziwi amekuwa akimtumia fedha licha ya kwamba yuko gerezani.
“Ananitumia fedha, anasema kuwa huwa wanafanya kazi wakiwa gerezani na kulipwa,” alimalizia.
Source:Global Publishers
MAMA WA BINTI KIZIWI AFUNGUKA KUHUSU KIFUNGO CHA MTOTO WAKE HONG KONG
8
August 21, 2013
Tags
Umaskini kweli mbayA yaani mama anavozungumza as if bintie alichofanya ni kitu sahihi kabisa.
ReplyDeleteWazazi wetu wengi wa kiAfrika wanatuza kwa maslahi yao wenyewe dear.. wazazi wetu wakiAfrica nikitu bora kuliko utu! Yaani angalia huyo mama anavyo ongea kama vile nothin hapen, yeye anajali mwanae anamtumia pesa tu. UMASKINI ULAANIWE !!
DeleteBijou
Unajua wanashangaza mama anasikitika utafikili alikuwa anafanya la maana.au kasingiziwa wa mama wengine wanataka umaarufu kupitia watotowao .acheni hizo
DeleteUmaskini kweli mbayA yaani mama anavozungumza as if bintie alichofanya ni kitu sahihi kabisa.
ReplyDeletePole mama hayo yataisha 2
ReplyDeleteMmh yuko proud na mtoto wake kufungwa huyo
ReplyDeleteLolest yaan mama karidhika kabsa nahc anataman aendelee kubaki hukohuko ili aendelee kumtumia fedhaaa wapi zed anto dunia haitaki fujoo ukileta za kuleta inakutupa kando! Ndo maisha tunajifunza kupitia makosa kaka vp taarabu inalipa?
ReplyDeletehivi lolest ina maana gan?mim nafaham....LOL(Laughing Out Loudly)
ReplyDelete