MANGULA NDIO AMEKWISHA KABISA KISIASA ?

Baadhi ya wanaCCM tuliamini kuwa kurudi kwa Philips Mangula katika medani za juu za uongozi wa CCM kungeleta mwamko mpya, mabadiliko makubwa na hamasa kubwa kwa CCM, lakini hali imekuwa tofauti kabisa.

Mangula hana kazi yoyote ya maana ambayo amefanya ndani ya CCM mpaka sasa, lakini pia kifikra na kujieleza Mangulla amechoka sana kama tulivyomshuhudia jana kwenye runinga wakati wa mjadala wa kipindi cha Uzalendo.

CCM ndani kwa ndani tumechoka mno na kwa nje tunazidi kuchokwa zaidi. Binafsi sioni hatua zozote za maana zinazofanywa na viongozi wa juu wa CCM hususani Philips Mangula kunusuru hali hii.
Je, hali hii inaashiria kwisha kabisa kisiasa kwa Mangula?

Source:Jamii forums
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad