"MAUAJI YA SOWETO YALIPANGWA NA KUTEKELEZWA NA POLISI" LEMA

Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto Arusha na kusababisha vifo vya watu wanne.

Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.

Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.

“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema



Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu Kama Hawa ndio Mnataka waongoze nchi haya

    ReplyDelete
  2. Yes, kuna logic kama unafuatilia sakata hili ka karibu, kama unafuatilia kwa kusoma magazti ya Chama Uhuru na Mzalendo tu, kalaghabao! Jamaa wana kitengo cha propaganda na Tambwe Hiza ndie kiongozi huko, sasa hawa waema kweli hamuwataki kwa kuwa mko addictive na propaganda, ushahidi wa video wa mauwaji ya Ars ya mwanzo yalionyeshwa bungeni? why? na haya sasa je? acheni kukumbatia hata vinavyonuka!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad