Mwnyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.
Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.
Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.
Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.
“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.
“Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.
“Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali.
“Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe,” alisema.
Kiongozi huyo alisema wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.
“CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa,” alisema.
Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.
Imetulia..endelea kupigania haki..usiogope mbowe.
ReplyDeleteMungu atakupigania baba
ReplyDeleteMti wenye matunda ndio upigwao mawe, endeleen kuwatetea watz, ila tunahitahi aman idumishwe cku zote
ReplyDeleteUSIJALI MKUBWA; 2015 SI MBALI NA MABADILIKO YATAFANYIKA TU KAZA MOYO KONDE
ReplyDelete