Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.
Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.
Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.
‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote’ alisema Subira.
Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.
Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.
CHANZO JAMBO TZ
Mwenyeezi Mungu amlipe Pepo huyo Kijana inshallah Wanachama Wenzangu Semeni Ameen.
MTU MMOJA ASIYEJULIKANA AGAWA PESA BURE BURE JIJINI DAR
11
August 19, 2013
Tags
Kapata wapi pesa mpaka agawe,kama za halali kwann hajitambulishi au haendi vtuo vya watoto yatima au atoe kwenye nyumba za Ibada,? .
ReplyDeletemtu unapotoa hutakiwi kujitangaza kwani unapojitangaza ni kufanya riya huko
DeleteNdio inavyotakiwa unagawa Pesa bila kupiga Picha au Mtu kujua.
Deletevizuri sana, sio wote wanapenda kujulikana wanapotoa msaada. kama ni a halali basi tumuombee Mungu amzidishie zaidi, kama sio za halali basi tumuombee pia ili asitumie jasho la wengine kujinufaisha.
ReplyDeleteNaomba ratiba yake, leo anapita wapi?
ReplyDeletebora asijitangaze manake watz hamchelew mtaanza oh anauza unga wakat mnahitaji kusaidiwa uje na mwanza jembe
ReplyDeleteApite na huku kwetu Tbt nyumba za kupanga wengine kodi zinakaribia kuisha...
ReplyDeleteduuu mdau umeua aje atulipie kodi jama mi niko mbezi atapita lin sijui
DeleteWe anony hapo juu kabisa acha zako, huwezi kumpangia mtu matumizi, ni zake anatoa anapotaka,fala we.
ReplyDeleteMatusi ya nn xaxa wkt nayeye kachangia? Fala mwenyewe nguruwe jike ww
ReplyDeleteWe umejuaje km haendi kutoa kwa watoto yatima. Dini gani ilisema m2 akitoa msaada aweke na mabango. Uko kutakua kutoa msaada au kujitangaza. Acha kutuletea elimu yako ya chini ya mwembe apa
ReplyDelete