Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana alikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa picha ya namna mchezo wa usafirishaji wa madawa ya kulevya unavyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Dr. Mwakyembe akionesha picha ya Masogange aliyoipost Instagram ikimuonesha ameshika lundo kubwa la hela
Mwakyembe alisema kamera za CCTV, zilizowekwa uwanjani hapo zinaonesha mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema majira ya saa 10:15 walionekana Agnes ‘Masogange’ Gerald akiwa na mdogo wake Melisa Edward walionekana wakiwa na mfanyabiashara mmoja katika eneo la kuingilia abiria huku wakiwa na mizigo na mabegi tisa yaliyofanana.
Alisema kamera zilimwonyesha askari polisi akihangaika kuwasaidia abiria mbalimbali kuweka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi, kazi ambayo alieleza kuwa haikuwa yake.
“Mbeba mizigo anayetuhumiwa kuwa katika mtandao huo alionekana akiwasaidia vijana hao watatu (Agnes, Melisa na mfanyabiashara) kupeleka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi na baadaye kuyazungushia mabegi hayo katarasi za nailoni na kuyafikisha kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini,” alisema.
Alisema kamera hizo zilimnasa ofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA akimwondoa katika kiti cha ukaguzi wa mizigo mfanyakazi mwenzake, na kukaa yeye ikiwa ni dakika chache kabla ya mabegi tisa ya vijana hao hayajaingia katika mashine ya ukaguzi.
“Kinyume na taratibu ofisa huyo hakujiandikisha kwenye kitabu cha wakaguzi (Screener’s logbook), saa 10:16 akaanza kupitisha mabegi hayo tisa mpaka saa 10:22. Alipomaliza kupitisha mizigo hiyo kwa dakika sita akamwachia ofisa aliyekuwa katika eneo hilo na kuondoka.”
Dr Mwakyembe alidai ofisa huyo baada ya kuondoka katika kiti hicho alizungumza kwa dakika kadhaa na askari polisi anayedaiwa kuwa katika mtandao huo na kurejea tena sehemu aliyokaa ofisa mwenzake wa TAA na kumnong’oneza jambo fulani.
“Baada ya hapo akaelekea ukumbi wa abiria huku akiongea na simu, mambo hayo yote yalifanyika huku kiongozi wa sehemu ya ukaguzi akiwa hapohapo bila kushtuka.”
Alisema baada ya mizigo hiyo kupita katika mashine ya ukaguzi (baggage screening machine), vijana wale watatu wakahamia na mizigo yao kwenye kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
“Mabegi matatu ya kilo 20 kila moja yalipitishwa yakabaki mabegi sita ambayo yalitakiwa yalipiwe malipo ya uzito wa ziada. Kwa taratibu za shirika hilo kila kilo moja inayoongezeka hulipiwa dola 5 (Sh8,000), vijana wale walitakiwa kulipia dola 600, lakini walitozwa dola 94 tu ambazo zinathibitishwa na risiti tuliyonayo,” alisema.
Alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia gharama ya dola 60 (Sh96,000) ili kupata tiketi.
“Kutokana na hali hiyo mhakiki wa nyaraka za safari nje ya ukumbi wa abiria siku hiyo, hakupaswa kumruhusu mfanyabiashara kuingia ndani ya ukumbi bila tiketi ya siku hiyo,” alisema na kuongeza; “Kwa hali ya kawaida mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa, lakini siku hiyo mbwa walichelewa na walikuja kutumika baadaye ikiwa ni baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.”
Alisema siku ya tukio saa 9:28 kamera hizo za usalama zilimwonyesha mbeba mizigo wa uwanja huo akiwa anazungukazunguka eneo la kuingilia abiria kama mtu ambaye ana ahadi na kukutana na mtu fulani.
“Kamera pia zilimnasa ofisa mwingine wa TAA kwa mara kadhaa akitoka na kuingia ndani ya jengo la abiria huku akizungumza na simu, kitendo ambacho hakiruhusiwi kabisa kwa wafanyakazi wa eneo la ukaguzi wa abiria,” alisema na kuongeza;
“Wakati huohuo, kamera zilikuwa zinamwonyesha askari polisi anayetuhumiwa kuhusika katika mpango huo akiwa anarandaranda eneo la uhakiki wa hati za kusafiria kama vile anasubiri kitu fulani.”
Kutokana na hali hiyo, Dr. Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kuwasaidia Masogange na mwenzake kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini, “Akamatwe na kuunganishwa na kesi inayowakabili Watanzania hao wawili.”
Alisema TAA inatakiwa kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi wake wanne waliohusika katika mpango huo, kuwakamata na kuwaunganisha katika mashtaka yanayowakabili.
Source: Mwananchi,
MWAKYEMBE ASIMULIA JINSI AGNESS MASOGANGE NA MDOGO WAKE WALIVYOPITISHA MADAWA YA KULE JNIA
3
August 17, 2013
Tags
Apo poa ila mbona hajataja vigogo aliowasema!
ReplyDeleteTunataka utaje wanaowatuma.
ReplyDeletewote ndo hao hao anatajwa aggnec tuu vigogo hawatajwi
ReplyDelete