NCHEMBA ATUHUMIWA KUSHUSHA HESHIMA YA CCM MBELE YA UMMA NA KUCHANGIA MATOKEA MABAYA

MATUKIO kadhaa ya kisiasa, mwelekeo, kauli na mienendo ya baadhi ya wanasiasa waandamizi na wenye nguvu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) vimeibua mkanganyiko na hali tete ndani ya chama hicho, Tanzania Daima Jumamosi limebaini.

Kwa muda sasa, kumekuwa na minyukano ya ndani kwa ndani miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM, huku baadhi yao wakilaumiana kwa “kuchafua na kuua” chama.

Baadhi yao wamefikia hatua ya kumlaumu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwapa madaraka makubwa baadhi yao, na kushindwa kuwanyang’anya pale wanapoonyesha dalili za “kuua” chama chao.

Gazeto hili linazo taarifa za baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM kupeleka ujumbe mzito kwa Makamu Mwenyekiti, Phillip Mangula, wakionyesha kukerwa na kauli au mwenendo wa baadhi ya viongozi waandamizi, hasa Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba.

Wanamtuhumu Nchemba kwa kushusha heshima ya CCM mbele ya umma, na kuchangia matokeo mabaya katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika Arusha mwezi uliopita, ambako CCM ilishindwa na CHADEMA katika kata zote nne.

Baadhi ya wazee na makada waandamizi wanasema Nchemba ni “mzigo wa Kikwete,” kwa maana kuwa ndiye aliyempa madaraka, na ndiye anayemsikiliza na kumpa jeuri.

Nafasi anayopewa Nchemba imeleta mgongano wa chini kwa chini kati yake na Katibu wa itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye kwa muda sasa amekuwa ndiye kipenzi cha Rais Kikwete katika kutekeleza mikakati kadhaa na kutoa matamko yenye utata dhidi ya viongozi au wanachama “wasiopendwa” ndani ya chama hicho, au dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa mujibu wa makada wanaokerwa na tabia ya Nchemba, kiongozi huyo amegeuka kero kwa viongozi wenzake, ambao wanasema ameingiza siasa za ujasusi wa waziwazi na mbinu nyingine chafu za kisiasa zinazomfanya aibomoe CCM na kuiongezea umaarufu CHADEMA mbele ya umma.

Source:Tanzania Daima
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera NCHEMBA usirudi nyuma na mikakati yako ,fanya lile unalolihisi lina tija kwa chama na wewe binafsi hao wengine ni waropokwaji ,wewe ni kijana mwenye uwezo wa kumudu hali halisi ya kisia kwa njia yeyote ile tumia uwezo uliopewa kichana na kitakulinda kwa nguvu zote

    ReplyDelete
  2. endelea kuua chama wenye uwezo waje kuongoza mmekalia kuuwa wananchi na kuwanyima haki zao za msingi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad