RAIS KIKWETE KAMATA MAFISADI WATANZANIA WAPUMUE TUMECHOKA

Kutokana na hali ya ufisadi nchini ilipofikia sasa, kwa maoni yangu ipo haja kwa Rais Jakaya Kikwete kuwatuliza Watanzania kwa kutenda jambo ambalo halijawahi kutokea kwa kipindi kirefu.

Watanzania wengi wanaamini kwamba Rais Kikwete ni muumini mzuri wa dini, anajali hali za watu, ni kiongozi makini, lakini wanakata tamaa kutokana na kasi ya ufisadi inavyozidi kushika kasi katika Serikali yake.

Ufisadi kwenye halmashauri nchini sasa unatajwa kuwa ni kama chama kikuu kilichojipanga kuiangusha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pamoja na wakurugenzi wengi wa halmashauri kushughulikiwa, lakini ukweli ni kwamba ufisadi umekithiri serikalini.

Kutokana na hali hiyo, ni wakati mzuri kwa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kuwakamata mafisadi wizarani, mikoani, wilayani hadi vijijini.

Rais achukue hatua ikiwamo ya kuwataka warudishe fedha zote ndani ya muda maalumu. Wakabidhi kwa serikali ‘mahekalu’ yote yaliyojengwa kwa ufisadi. Pamoja na kwamba wamejenga kwa majina ya watoto, wajukuu na hata ndugu wengine, lakini wajisalimishe na kujieleza ni jinsi gani walivyopata fedha.

Kwa wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi mpya, Rais aseme neno likiwamo la kuwataka wajibu hadharani mbele ya Watanzania kupitia vyombo mbalimbali vikiwamo vya habari na hatimaye kuwapeleka kortini.

Ikumbukwe, Watanzania wengi wanaipenda Serikali iliyoko madarakani.

Watanzania wamesikia mambo ya watumishi wa Serikali kukamatwa na nyara, mambo ya Bandari, Mambo ya Wizara ya Mambo ya Nje, ufisadi ujenzi wa barabara ambako ufisadi umesababisha gharama za ujenzi kuwa kubwa. Kilometa moja ya lami sasa inakaribia Sh1 bilioni bila sababu za msingi.

Wizi mwingine wa mafisadi sasa ni wa maandishi kwa kuongeza cha juu kuanzia Sh100 milioni na kuendelea hadi mabilioni. Viongozi waliopewa dhamana wanapokubali kila kitu wanachoambiwa na wataalamu wao hususan masuala ya fedha, ni wazi wanaruhusu ufisadi. Kikwete atoe neno sasa.

Taarifa za ufisadi zinaripotiwa kuanzia wizarani, mikoani, halmashauri hadi vijijini. Hata mwanasheria mkongwe wa kimataifa, Nimrod Mkono anaamini kwamba asilimia 60 ya fedha za Serikali kwa ajili ya kununua madawati zinaishia kwenye mikono ya watu binafsi. Rais kamata wanaotajwa kuhusika.

Mkono alinukuliwa na gazeti hili akisema ufisadi kwenye fedha za Serikali ni balaa. Kwa hali hiyo Rais anaweza kuwatuliza Watanzania kama atatenda lolote zito dhidi ya watu wanaotuhumiwa.

Jambo la kusikitisha ni kuona kwamba mafisadi hayo sasa yameingia mpaka Ikulu ambako nako wakisikia Rais atafanya ziara nje ya nchi wanaweka mikakati ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kujinufaisha.

Kwa mfano tukio la karibuni ambalo ni la kusikitisha ni Sh8 bilioni zilitumika kwa mkutano wa siku tatu.

Waziri Sitta alishauri Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ichunguze kashfa ya matumizi tata ya fedha hizo zilizotumika wakati wa Mkutano wa Smart Partnership Dialogue ulioshirikisha viongozi kadhaa wa Afrika sambamba na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama.

Kwa kuwa suala hili sasa lipo hadharani, mawaziri husika bila kushinikizwa wanatakiwa kutoa maelezo kwa vyombo vya habari juu ya matumizi halali ya fedha zote hizo. Kama hawataki basi Rais awashinikize wafanye hivyo ili kuisafisha Serikali ya CCM. Bila Rais kuchukua hatua, uchaguzi ukiwa wa haki mwaka 2015, kazi ipo kwa CCM.

Source:Mwananchi
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawezi huyo!...yeye mwenyewe mshirika!Otherwise ni nn chamfunga mikono na midomo.Atajing'ata!

    ReplyDelete
  2. Yeye mwenyewe fisadi mshezi tu huyo fisadi wao wa kwanza nyerere ajamariza mafisadi hata wamaliza yeye

    ReplyDelete
  3. natamani nyerere angekuwepoooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. That is my wish too baba wa taifa he was just honestly president tanzania ever,We umesikia wapi uwataje wezi wakati wemwenyewe ni jambazi..SHAME ON YOU ALL such a pit kwa wananchi wa kawaida wa tanzania ambao ata wengine kula yao ni matata but viongozi wa nchi they just play with millions..That is real PAIN and GOD MAY PANISH YOU ALL IN TIME.

      Delete
    2. Nyerere angerudi angekufatena maana hali ni tete

      Delete
  4. Labda aanze kujitaja yeye kwanza na wengine watafuata, he is the No 1 TZ corrupt kupitia mwana RIZ.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad