Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limelaani vikali tukio la polisi kumjeruhi Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu, Sheikh Issa Ponda na limetaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza tukio hilo huku likimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kujiuzulu.
Ponda amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), akitibiwa majeraha yanayoaminika kuwa ya risasi aliyoyapata Ijumaa iliyopita mkoani Morogoro.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema baraza hilo limesikitishwa na tukio hilo na kusisitiza kwamba, uchunguzi huru unahitajika ili kuhakikisha kuwa wahusika wote wanakamatwa.
“Ieleweke kwamba Bakwata na Sheikh Ponda siyo maadui. Tunatofautiana mawazo tu, linapotokea suala lisilo la haki za binadamu lazima tuwe kitu kimoja,”... Sisi Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, tumesikitishwa na tukio hilo, tunataka tume huru ya kuchunguza kifaa kilichomjeruhi na kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria. Polisi walitakiwa kutumia njia ya weledi katika kumkamata, lakini siyo kumjeruhi kama ilivyotokea.”
Alisema Bakwata inamtaka Shilogile kujiuzulu mara moja ili kupisha tume huru itakayoundwa kuchunguza kwa ufasaha juu ya kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.
Alisema: “Hata kama Sheikh Ponda anatafutwa na polisi, ungetumika weledi wa kumkamata siyo kumjeruhi. Tunaamini polisi ina mbinu nyingi za kuwakamata wahalifu na Ponda kazunguka mikoa mingi ikiwemo Zanzibar walishindwaje kumkamata!” alihoji Sheikh Salum.
Alisema ikithibitika kwamba Sheikh Ponda alijeruhiwa kwa risasi au polisi walihusika, hatua kali zichukuliwe kwa wahusika kwa sababu tukio hilo linahatarisha usalama wa nchi.
Kauli ya Sheikh Salum inafanana na ile iliyotolewa na juzi na Amiri wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Yusuf Kundecha ambaye aliitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza tukio hilo.
Hata hivyo, Polisi imeipa jukumu Kamati ya Haki Jinai chini ya Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu kuanza kazi ya kuchunguza tukio hilo.
Hatua ya polisi kuanza kuchunguza tukio hilo imepingwa vikali na Sheikh Kundecha ambaye jana alisema haiyumkiniki kushiriki kuchunguza tukio hilo wakati yenyewe inatuhumiwa kuhusika.
“Umeona wapi mtu anampiga mtu halafu huyohuyo anaunda tume eti kuchunguza kipigo na aliyepiga anakuwa ndani ya tume... hii ni sawa na Tume ya Mwangosi ambayo haikuja na majibu. Kinachotakiwa ni kuundwa tume huru ikiwashirikisha Waislamu,” alisema.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema jana kuwa Kamati ya Haki Jinai imeshaanza kazi juzi ya kufuatilia tukio hilo kazi kubwa ikiwa ni kuchunguza namna lilivyotokea ikiwa ni pamoja na mazingira yake.
PENGO ALILOLIACHA MSAIDIZI WA MUFTI SIMBA SHEHE GOROGOSI LINAONEKANA WAZI SASA HIVI WAISLAMU WENYE SIASA KALI WANATAKA KUIANGUSHA BAKWATA NI MAAFA KWA TAIFA NI MWISHO WA AMANI NA UTENGEMANO
ReplyDeleteBakwata acheni unafiki wasenge nyie
ReplyDeleteUctukane ndugu yangu.unahisi ndo suluhisho?
DeleteWanausalama sasa ni wadunguwaji
ReplyDeleteMussa kumbuka maneno yako katika Gazeti la mtanzania tarehe saba mwezi hu
ReplyDeleteKuunga mkono kwa bakwata ni jambo jema,sasa mnatakiwa kuunga mkono harakati za kiislam za shekh ponda,muislam kuswaliswali tu haisaidii,mungu atujaalie watanzania tutambue iman yetu kikwelikweli
ReplyDeleteBakwata achen ku2mikia ukafr rejeeni kw allah s.w.. Muogopen allah
ReplyDeleteWanausalma watakua hawa bwn. M/mumgu ndo mwenye jeshi la wamausalama la malaika watiifu. Hawa wanausalama au wanauhasama?? Eti usalama wa taifa pphooo usalama wa taifa au usalama wa chama chama
ReplyDelete-ccm-
Maofisa wanyamapori. Pgen 2 lakn kumbken c nyie peke yenu mnaeweza ku2mia silaha 2kishazitia mikononi 2tafumuana 2.
ReplyDelete