SERIKALI YA RWANDA IMEAPA KUTOWAFUKUZA WATANZANIA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania. 

Akizungumzia sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.

Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.

Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k

DW - Kiswahili

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Poleni sana wananchi wa Rwanda mliokuwa Tanzania, dharau na kejeli za rais wenu Kagame ndio zinawaponza nyinyi kufukuzwa kama mbwa.

    ReplyDelete
  2. Hakuna wahamiaji haramu wa kitanzania huko Rwanda; ni wale waliokaribishwa na serikali ya Rwanda ili kusaidia katika majukumu ya kitaalamu, na huwa wanarudi nyumbani kila mwaka bila wasiwasi wowote. Wakiambiwa waondoke wanarudi bila tatizo lolote kwani hawako kule Rwanda kama "NYUMBANI" bali wako kule kama wasakaji tu.

    ReplyDelete
  3. Mda c mrefu balozi WA tanzania Rwanda,atarudishwa nyumbani tz,hapo ndo ujinga WA kiwete president,unapotuletea matatizo,as a soldier cwez pigana vita ya kujitakia kwa kimdomo cha rais mburula

    ReplyDelete
  4. acha ufala wewe ,kila kitu mnataka kuweka dosari mbona wewe huweki wageni usowajua nyumbani kwako?

    ReplyDelete
  5. ACHA UKENGE WEWE KAMA UNAONA RAIS KAKOSEA BAS WACHUKUE HAO WANYARWANDA WAKAE NYUMBAN KWAKO NYAMBAFFFFFF

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad