JAMES Hussein, mkazi wa Kimara, Dar
alikuwa na wakati mgumu wa kukwepa kamera zilizotua Mahakama ya Wilaya
Ilala, jijini Dar juzi baada ya kufikishwa kwa kosa la kujifanya
trafiki.
Tukio hilo lilijiri mahakamani hapo
Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa alikana mashitaka mbele ya Hakimu
Mfawidhi, Joyce Minde.
Trafiki feki huyo alitumia muda mwingi
kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini alichemsha kwani kila
alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele yake.
Hali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana.
Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha
Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema mnamo Agosti 14, 2013,
huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar, mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo
za askari wa usalama barabarani akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la
polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa
rumande Segerea, hadi Septemba 5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili
kwa shilingi milioni kumi na nne.
VIOJA VYA TRAFIKI FEKI MBELE YA HAKIMU MFAWIDHI -ILALA
1
August 25, 2013
Tags
maskini alikuwa anatafuta tu maisha nayeye maskin mngemuachia tuu dii
ReplyDelete