WATOTO WA KIKE, TUWAFICHE WAPI WASIYAONE MAPENZI?

Mwanzoni mwa juma hili,nilitembelea shule moja ya wasichana nikiwa na shida ndogo ya kiofisi hapo.
Jina la shule naomba nilihifadhi sina taaluma ya uandishi wa habari,nisikiuke misingi yake.
...
Nilipofika ofisini nilikaribishwa staff ya walimu,nikaambiwa nisubiri.Hapo ndipo niliduwaa kumuona mwalimu mmoja wa kike akiingia ofisini na mtoto wa kike,kidato cha tatu huku akiandamwa na fimbo za mgongoni.
...
Tatizo lilikuwa kwamba,,yule binti alikuwa amekamatwa jumapili yake(siku iyo ilikuwa jumatatu)
Akiwa amelala na wanaume wawili wakati wenzake wameruhusiwa kwenda nyumba ya ibaada.Shule yenyewe ina taratibu ya kuwaruhusu wanafunzi kuhudhuria ibaada nje ya shule ambapo ni mwendo wa dk 25 ivi kwa miguu... Mwanafunzi huyu alikiri kulala na wanaume hao wawili na alipoulizwa aliwafaham vipi,alisema alitumia simu ambayo pamoja na shule kuzuia bado aliiweka kwenye taiti,,ikiwa na vibration.Aliweka wazi kuwa matroni hata akague vipi hawezi kuwakamata wote maana wanafunzi wengi wana simu.
...
Alipoulizwa anapaje ujasiri wa kulala na wanaume wawili,huku akilia anasema alikubaliana na mmoja,akaongezeka wa pili,,hivyo asingeweza kuwazuia.
...
Tukio hili ambalo bado linaendelea kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo wahusika kutafutwa,,lilinifanya niondoke na maswali mengi kichwani.Je tuwafiche wapi? Je malezi gani tuyatumie? Je wazazi walio nyumbani wanajua watoto wao wanamiliki simu? Je imefika mahali,somo la Mahusiano Urafiki Mawasiliano na Mapenzi liwekwe shuleni? Je hawa ndo wake wema na waume wema wa kesho?
Iliniuma,,jamani tusitafute wa kulaumu bali nini kinaweza kuleta usalama.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania tumeharibiwa sana na ulimbukeni. Mambo yote yanayotumiwa kama visingizio yaani teknologia ya TV, simu, SMS, email na sinema, vipo pia katika nchi nnyingine. Kwa mfano Marekani ndiko kwenye makolezeo lakini utashangaa sana ukiambiwa kuwa asilimia kubwa ya wasichana wa kimarekani huwa hawajalala na mvulana yoyote kabla ya miaka 21 wanapokuwa college mwaka wa pili. Watoto wanaovurugikiwa na maisha ni wale walio na malezi mabovu ya kutokuwa na wazazi makini, kama wale wa inner cities. Tatizo letu Tanzania ni malezi tu. Wazazi wa kitanzania wanawaacha watoto wao mapema sana, ama kwa visingizio vya shule za bodingi, au kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulea wanawaacha watoto wajitafutie maisha mitaani. Kwa hiyo watoto wanaharibika kwa kunyimwa malezi na wazazi wao.

    ReplyDelete
  2. hili nijanga na sijui tutanusuru vipi vizazi vyetu malezi mabovu huchangia lkn wakat mwngn si malezi jmn niwatt na magroup yao wanayokutana nayo huko mashuleni ht wa day school tatizo ni hilohilo. M.mungu atusaidie awasaidie nakuwalinda hawa wtt ukizingatia tupo kwenye ulimwengu wa maradhi na wtt wadogo wanajiingiza ktk mapenzi naona tunatengeneza taifa la wafu na sivinginevyo..... inauma sana na kusikitishi

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana. Sijui tufanye nin. Unawaombea dua kila siku lakini mambo ya ajabu kila siku. Ningependa kama watoto wangeenda bording wakiwa sekondar na si primar nadhan uhuni ungepungua maana wengi hujifunza mapenz kwa kuiga wenzao lakin wangeishi na wazazi umri wa chini wangefunzwa mazur na mabaya.

    ReplyDelete
  4. Walimu wenyenyewe hovyo , wazazi hovyo sasa wanafunzi watazuiwaje na haya mambo? Ushauri wangu waachwe watombe au watombwe mpaka basi, kikubwa wakadhaniwe matumizi ya Kondom that's solutions.

    ReplyDelete
  5. huo ndo mwisho wa dunia kikubwa kumwomba Mungu.

    ReplyDelete
  6. Ni vigumu sana wazazi wenyewe wakutana katika hali kama hizo au kuliko hizo na watoto nao wanazaliwa katika mazingira wanawaona wazazi wao wanyo yafanya inahitaji Serekali kuweka sawa ikifanya hivyo kwa kuweka adhabu kali basi kila mtu atakuwa na heshima lakini viongozi wenywe ndio wenye mapenzi na hayo mambo

    ReplyDelete
  7. huo ni umalaya wao.. Wazazi wasisingiziwe maana mitoto yenyewe imekubuhu kabla hata ya wakati muafaka. Gari likiwaka limewaka 2 hata iweje tabia zao hizo ndio zao hawawezi kubadilika.

    ReplyDelete
  8. wanasema samak mkunje angali mbich minaona malez nyumba zakupanga babamama watoto chumba kimoja washindwa kufanya hayo nawengine tamaa hasa watoto wakike anga lia mtoto anasim ya laki3 mazaz hashangai wakat uwouwo yeye ana sim ya tochi haya mambo kuisha siyo lais 2jitaid kuwakunja watoto wetu angali wabich
    usimuonyeshe saaana matenzi mtotowako hadi kufia kuku zoeya atakua hakuogop nasemea wakina baba pamoja na wakinamama

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad